25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Ugonjwa wa TB wadhibitiwa migodini

Aveline Kitomary – Kilimanjaro

HOSPITALI ya magonjwa ambukizi ya Kibong’oto imefanikiwa kupunguza kiwango cha maambukizi ya ugonjwa Kifua Kikuu (TB) huo katika maeneo ya migodi madini  kutokana na kampeni za uelimishaji  zinazotolewa katika maeneo hayo.

Hayo yalisemwa jana mkoani Kilimanjaro, wakati wa ‘Kampeni za Tumeboresha Sekta ya Afya’,  iliyoandaliwa na maofisa habari kutoka taasisi zilizoko chini ya Wizara ya Afya na Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk. Donatus Tsere, ambapo alisema wagonjwa wengi walioko katika maeneo hayo sasa wanapata matibabu kwa wakati.

“Tumeanzisha kliniki maalumu kwaaajili magonjwa ambukiza na kifua kikuu kwa watu walioko katika maeneo ya shughuli ya kazi hasa migodini  ambayo imeanza mwaka 2018 inahudumia hasa wachimbaji wa madini Mirerani.

“Matokeo yake ni kwamba hata uibuaji wa kifua kikuu katika migodi hiyo imeongezeka kwa asilimia 14 ukiweka katika takwimu ni sawa na wagonjwa 14,000 kati ya watu 100,000.

“Wameongezeka baada ya kufanya kampeni katika maeneo hayo ya kuhamasisha kuja kupima kulingana na mazingira yao kwani huwa wako makundi na kunavumbi huko halafu huko shimoni hewa kidogo hivyo tunawafanyia vipimo kila baada ya miezi mitatu,” alisema Dk. Tsere.

Alisema kutokana na kuendelea kuboreshwa kwa huduma za maabara, uwezo wa kubaini wagonjwa wa kifua kikuu umeongezeka kutoka wagonjwa 120 mwaka 2015 hadi wagonjwa 480 kwa mwaka 2019.

“Hatua hiyo pia imekuja baada ya  vituo vya huduma za kifua kikuu kuongezeka na kufikia 145 kwa nchi nzima hii inaleta urahisi wa mgonjwa kutibiwa katika eneo lake.

“Pia tunafanya utafiti wa kufupisha matibabu ya  kwa kutengemeza dawa ya muda mfupi kwa kuchanganya dawa karibia nne hizo zimechanganywa na kutumika kwa muda mfupi,” alisema

Akizungumza mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka minne, alisema hospitali hiyo inaendelea na ujenzi wa maabara ya kisasa ambayo itakuwa na uwezo wa kupima virusi vya magonjwa ya mlipuko.

“Hospitali inaendelea kusimamia na kuendeleza mradi wa ujenzi wa maabara ya kisasa ya level 3 utakaokuwa na uwezo wa kufanya uchunguzi wa virusi vya magonjwa yote ambukizi kama virusi vya ebola, corona na vingine na ujenzi wake utagharimu Silingi bilioni 8 mpaka lakini mpaka sasa umekamilika kwa daraja la kwanza ambao umegharimu Sh bilioni  1.9 na mwezi huu tutakabidhiwa,” alifafanua Dk. Tsere.

Alisema mafanikio mengine ni maboresho makubwa katika maabara ambapo vifaa vya kisasa vya zaidi ya Sh milioni 300 vimenunuliwa  kwa ajili ya kufanya uchunguzi na kuangalia mwenendo wa matumizi ya dawa hivyo  wagonjwa wanapata matibabu mazuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles