Na Omari Mlekwa, Hai
MKUU wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amewataka wafanyabiashara wawili wa mabasi ya Machame Safari na Limu safari kujisalimisha katika kituo cha polisi cha Bomang’ombe kutoka na kuwepo kwa taarifa za kuhujumu miundombinu ya reli.
Wafanyabiashara hao waliotakiwa kuripoti kituo cha Polisi Bomang’ombe leo Jumapili Januari 19, 2020 kabla ya saa 10 jioni ambao Clemence Mbowe anayemiliki mabasi ya Machame Safari na Rodrick Uronu anayemiliki mabasi ya Lim Safari
Wamiliki hao kwa pamoja wanatuhumiwa kuunda genge la uhalifu kwa lengo la kuhujumu miundombinu ya reli ili kuathiri usafiri wa treni ya abiria kati ya Dar es Salaam- Moshi.
Sabaya alitoa agizo hilo baada ya kutembelea ukarabati wa ujenzi wa eeli katika kijiji cha Rundugai ambapo alisema kuwa kumekuwepo na taarifa za kuhujumu miundombinu ya Reli ambao unaendele kuelekea mkoani Arusha
“Nimepata taarifa kuwa kuna wafanyabiashara wawili wana genge la kuhujumu ujenzi huu ili kukwamisha juhudi za serikali za kurahishia wananchi usafiri na kuwapunguzia adha ya usafiri,” amesema Sabaya.