25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya kumwondoa Trump yaanza Seneti

WASHINGTON, MAREKANI

VIKAO vitakavyoamua iwapo Rais wa Marekani, Donald Trump anapaswa kuondolewa afisini vimeanza katika bunge la seneti nchini Marekani. 

John Roberts, Jaji mkuu katika mahakama ya juu ameapishwa kuongoza vikao hivyo. Maseneta ambao watakuwa kama majaji, hawaruhusiwi kuzungumza wakati wa vikao hivyo na lazima wawasilishe maswali yoyote kupitia maandishi. 

Baada ya Roberts kuapishwa, alitoa viapo kwa maseneta wote 100 vya kuzingatia haki.

Wabunge wawili wa chama cha Democratic kutoka kwa bunge la waakilishi wanaoongoza kesi hiyo dhidi ya Trump ni Adam Schiff wa jimbo la California na Jerry Nadler wa New York. 

Kundi la waendesha mashtaka saba pia linajumuisha wawakilishi kutoka Texas, Colorado na Florida. 

Baada ya mashtaka kusomwa na kila mmoja kuapishwa, vikao hivyo viliahirishwa hadi Jumanne wiki ijayo  ambayo itakuwa ni Januari 21 kwa kuwa bado kuna maamuzi ya usimamizi yanayopaswa kufanywa kuhusu jinsi vikao hivyo vitakavyoendelea.

Wiki zijazo, maseneta wataamua iwapo Trump anastahili kuondolewa madarakani kwa makosa yaliyowasilishwa na Bunge la Wawakilishi.

 YALIYOJIRI ALHAMISI

Vikao vya bunge la Seneti vilianza huku msimamizi wa Bunge akihakikisha shughuli za bunge ziko sawa (sergeant at arms). 

Vifungu vya kumwondoa Trump madarakani vilisomwa na mbunge wa Congress na mwendesha mashtaka mkuu Adam Schiff.

Schiff ni mmoja kati ya saba ambao watakuwa wanafanya maamuzi ya kesi dhidi ya rais. 

Alisema hakuna rais ambaye amewahi kuzuia mchakato wa kura ya kutokuwa na imani naye.

Chuck Schumer, Kiongozi wa Democratic katika bunge la Seneti, alitoa tena wito kwa mashahidi wapya kujitokeza na vilevile ushahidi wa nyaraka uruhusiwe bungeni. ”Kesi hii inahitaji uthibitisho wa wazi.”

Spika wa Bunge, Nancy Pelosi ametaka mchakato wa kesi kufanyika kwa haki.

Seneta Susan Collins wa Republican ambaye atakuwa na kibarua kigumu cha kuchaguliwa tena mwaka huu, alionekana akibubujikwa na machozi wakati mashtaka yanasomwa.

Wabunge waandamizi wa Democrats walimkosoa vikali McConnell baada ya kuahidi kushirikiana na rais Trump na kuonekana kama anayetengua kiapo walichoapishwa maseneta wa Republican cha kuendeleza kesi hiyo kwa haki na bila upendeleo.

Akizungumza baada ya vikao vya Alhamisi, Schumer aliwaambia wanahabari: “McConnell amesema kwamba yeye atashirikiana na rais, sisi hatutashirikiana na yeyote.”

McConnell hajaondoa uwezekano wa mashihidi kuitwa. 

Lakini alipendekeza kwamba hilo litakuwa ni sawa na kuigiza kesi ya kutokuwa na imani ya Rais Bill Clinton ya mwaka 1999, wakati ambapo maseneta walipiga kura ya mashahidi watakaoitwa na kufuatiwa na majadiliano makali na kipindi cha maswali yaliyoandikwa.

Wakati kikao hicho kinaelekea kukamilika katika eneo la Capitol Hill, Alhamisi, Trump aliwaambia wanahabari waliokuwa Ikulu kwamba kesi hiyo inastahili kumalizika haraka iwezekanavyo.

“Huu ni uwongo mtupu,” Trump alisema  na kuongeza;  “Madai ya undanganyifu yaliyotungwa na Democrats ili wapate kushinda katika uchaguzi.”

Democrats wanadai Trump alizuia Dola za Marekani milioni 391 (£299m) msaada wa kijeshi ili kushinikiza Ukraine kumchunguza mpinzani wake wa kisiasa, Joe Biden. 

Trump ni rais wa tatu kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye. 

Marasis wawili wa kwanza ni Andrew Johnson na Bill Clinton ambao hawakuondolewa madarakani.

Theluthi mbili ya maseneta inahitajika ili rais aweze kuondolewa madarakani.

Wakati ambapo Bunge la Seneta linaongozwa na Republican, Trump anatarajiwa kuondolewa mashtaka hayo.

Timu yake ya utetezi bado haijatangazwa, lakini mawakili ya Ikulu ya Marekani, Pat Cipollone na Jay Sekulow wameombwa kuongoza.

Bunge la Wawakilishi lilipiga kura Jumatano kupeleka madai ya kumwondoa madarakani kwa bunge la Seneti, baada ya kupiga kura ya 228 kwa 193.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles