27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Binti bilionea wa Dos santos kugombea urais Angola

LUANDA, ANGOLA

BINTI  wa aliyekuwa rais Angola,  Jose Eduardo dos Santos aliyeongoza taifa hilo kwa miaka 38, Isabel  Dos Santos, amesema huenda akagombea urais.

Isabel, mwenye umri wa miaka 46 ni miongoni mwa wanawake matajiri zaidi duniani, huku jarida la Forbes likikadiria mali yake kuwa yenye thamani ya Dola  za Marekani bilioni 2.2, hatua inayomfanya kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika.

Ingawa mara kadhaa huko nyuma amepata kukataa kuwania nafasi hiyo lakini katika mahojiano aliyoyafanya na televisheni ya Ureno amesema  kwamba kuna uwezekano atawania urais 2022.

Kauli yake hiyo ya kuwania urais imekuja katika wakati ambao anaandamwa na kesi ya ufisadi na tayari waendesha mashtaka wako katika harakati ya kukomboa Dola za Marekani bilioni moja (£760m) ambazo Isabel washirika wake wanadaiwa na serikali.

Yeye mwenyewe amekana kufanya makosa yoyote.

Wakati baba yake akiwa madarakani, katika hali iliyozusha utata mwaka 2016 alimteua kuongoza kampuni ya mafuta nchini Angola inayomilikiwa na serikali ya Sonangol.

Alifukuzwa kazi mwaka 2017 na rais Joao Lourenco , mrithi aliyechaguliwa na baba yake.

Katika mahojiano mjini London, aliwahi kuripotiwa akisema kwamba maisha yake yapo hatarini iwapo atarudi nchini Angola katika hali ilivyo sasa.

”Kuongoza ni kuhudumu, hivyo basi nitafanya ninachoweza maishani mwangu” , alisema na kufuta msimamo wake wa awali kwamba alikuwa hana hamu ya kufanya siasa.

Mahakama moja mjini Luanda mwezi uliopita iliagiza kufungwa kwa akaunti ya benki ya Isabel na biashara yake katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta, kutokana na chunguzi kadhaa kuhusu madai ya ufisadi uliofanywa dhidi ya na familia ya dos Santos ambayo waendesha mashtaka wanasema imelipokonya taifa hilo zaidi ya dola bilioni mbili.

Nduguye wa kambo, Jose Filomeno Dos santos anakabiliwa na kesi nchini Angola kutokana na mashtaka ya ufisadi.

Upande wa mashtaka unadai kwamba yeye na wenzake walisaidia kupeleka nje ya nchi Dola za Marekani milioni 500 wakati alipokuwa mkuu wa hazina ya Angola .

HUYU NDIYE ISABEL

Mbali na kuwa mtoto mkubwa wa Dos Santos, Isabel ni mke wa mfanyabiashara wa Congo, Sindika Dokolo.

Aliwahi kufanya kazi katika shule ya wasichana ya mabweni nchini England.

Alisomea uhandisi wa umeme katika chuo kikuu cha Kings College mjini London.

Akiwa na miaka 24 alikuwa akimiliki hisa katika mgahawa wa Miami Beach uliopo mjini Luanda.

Aliinuka na kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika, alichaguliwa kuongoza shirika kuu la mafuta nchini Angola la Sonangol mwaka 2016 na kufutwa kazi 2017.

Ana hisa za asilimia sita katika mafuta ya Ureo na kampuni ya gesi ya Galp ambayo ni thamani ya Dola za Marekani milioni 830.

Anamiliki 42.5% ya benki ya Portugal ya Eurobic bank

Ana asilimia 25% ya hisa katika kampuni ya simu ya Unitelnchini Angola

Pia ana 42.5% ya hisa katika benki ya Angola kwa jina Banco BIC

Isabel amekuwa akimshutumu mara kwa mara Rais Lourenco ambaye alimrithi babake.

Licha ya kutoka katika chama kimoja, cha MPLA Rais Lourenco amewashangaza wengi kwa kuonekana akiilenga familia ya Dos Santos kwa ufisadi.

”Iwapo kutakuwa na mgombea tofauti kabla ya uchaguzi mkuu wa 2021 ambaye ataungwa mkono na rais wa zamani Jose dos Santos ama washirika wanaohusishwa naye hiyo itatoa changamoto kuu kwa Lourenco kwa kuwa rekodi yake ni mbaya sana , ukosefu wa ajira , uchumi uliozorota na msururu wa migomo” ameeleza mmoja wa wachambuzi.

”Ukweli ni kwamba kuna ushahidi mwingi dhidi yake . Ni mtu muhimu katika familia ya Dos Santos na tisho kubwa kwa Lourenco”, alisema Daria Jonker ambaye ni mchambuzi

Jonker anaamini madai ya ufisadi yalikuwa yakitumiwa na Serikali kama mojawapo ya vita ndani ya chama cha MPLA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles