21.1 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Mabeste, Lisa walivyowaliza mashabiki wao

Betrice Kaiza

WIKI iliyopita katika safu hii tulikuwa na msala wa mwanetu rapa kutoka Mji kasoro bahari, Morogoro, Boniveture Kabogo ‘Stamina’, kuhusu mkasa wa kuvunjika kwa ndoa yake kutokana na mausla ya usaliti.

Jinamizi la kuvunja ndoa za mastaa limeendelea kutafuna mahusiano mengi baada ya wiki hii rapa, Venance William ‘Mabeste’ na  mkewe Lisa Karl Fickenscher kuweka wazi kuwa tayari wamepeana talaka.

Kapo hiyo iliyobeba maana halisi ya mapenzi ya dhati, kwa muda wa miaka saba ilifanikiwa kujizolea umaarufu uliokuja  kwa jinsi walivyoweza kuwa pamoja hasa katika nyakati ngumu za matatizo waliyokuwa yanawakumba.

Mashabiki wa Bongo Fleva wanakumbuka moja ya mapito magumu waliyowahi kupitia wawili hao ni mwaka 2015, ambapo Mabeste alitangaza kuomba msaada kwa jamii ili mkewe apate matibabu ya maradhi yaliyomsumbua kwa muda wa miaka miwili nyuma toka alipopata ujauzito wa mtoto wake wa kwanza.

Kapo hiyo yenye watoto wawili,  Kedrick na Kaylyn iliweza kuvuka mtihani huo baada ya Lisa kupona na maisha kuwawia magumu  upande wa fedha kutokana na kutumia muda mwingi kwenye matibabu.

Baada ya kupata nafuu wawili hao waliamua kufunga ndoa takatifu Oktoba, 2016 kisha ikafanyika halfa ndogo iliyofana na kuwakutanisha watu wachache jijini Dar es Salaam.

Hali hiyo ngumu ya maisha hasa upande wa fedha, ilifanya watimuliwe kwenye nyumba waliyokuwa wamepanga maeneo ya Goba, Dar es Salaam na kwenda kupewa msaada wa kuishi kwa kiongozi wa kanisa.

Uvumilivu katika hayo mapito, ulifanya watengeneze mashabiki wengi ambao waliitazama kapo hiyo kama ya mfano. Mara nyingi tumeshuhudia wanaume wakitelekeza wake na watoto wao pale ambapo wanapita kwenye wakati mgumu.

Ila kwa Mabeste na Lisa ilikuwa tofauti, walionekana kubeba changamoto zao kwa pamoja na kupambana nazo mpaka walipofanikiwa kuzivuka, jambo lililowaongezea mashabiki na kuwa kivutio kwa wengi.

Ndiyo maana Lisa alipotaka kuomba talaka, hofu kubwa kwa Mabeste ilikuwa watu watatuonaje? Tutawaambia nini watu hiyo yote ilitokana na ukweli kwamba kuvunjika kwa penzi hilo kungewaumiza wengi.

Ndivyo ambavyo imetokea wiki hii baada ya wawili hao kutangaza kuwa ni mwaka sasa toka walivyoachana kwa talaka. Wamejikuta wakiwagawa mashabiki wao, wapo waliokuwa upande wa Mabeste kwa kumpongeza jinsi alivyoweza kumsimama mstari wa mbele kipindi mkewe anaumwa.

Pia wapo watu wanaompongeza Lisa kumuacha Mabeste na kwenda kwa bwana mwingine ambaye alikuwa ni rafiki wa familia yao na wengine wamebaki njia panda wakiwaombea wawili hao warudiane tena jambo ambalo mpaka sasa linaonekana ni ngumu kwao.

Sababu kila mmoja tayari ametangaza kuwa kwenye mahusiano mengine licha ya watoto wao kuwa kiunganishi kikubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,592FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles