28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Adaiwa kumuua mwanawe baada ya kujisaidia kitandani

Nyemo Malecela -Kagera

JESHI la Polisi mkoani Kagera linamshikilia Juma Daniel  (30), kwa tuhuma za kumuua mtoto wake Bahati Juma (2) kwa kutumia kitu cha ncha kali baada ya kujisaidia haja kubwa kitandani.

Tukio hilo lilitokea usiku wa Desemba 27 mwaka jana maeneo ya Rubanga ‘A’, Kijiji cha Kazingati, Kata ya Keza, Tarafa ya Rulenge, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Revocatus Malimi alisema usiku huo, Daniel ambaye ametengana na mzazi mwenzake, alikuwa amelala na mwanamke mwingine, Emilian Juma (28) pamoja na mtoto huyo.

“Baada ya mtoto huyo kujisaidia haja kubwa kitandani, baba alimchoma choma moto kwa kutumia kitu cha ncha kali usoni, makalio, sehemu nyingine za mwili na kumwingizia kitu hicho sehemu za haja kubwa na kumsababishia majeraha makali.

“Mbali na baba huyo kumjeruhi vibaya mtoto huyo, bado haliendelea kumficha ndani na kuendelea kumtibu kwa miti shamba hadi afya ya mtoto ilipokuwa mbaya zaidi ndipo mtuhumiwa aliamua kutoroka,” alieleza Kamanda Malimi.

Alisema baada ya baba wa mtoto kutoweka nyumbani, majirani walisikia sauti ya mtoto huyo akiomba msaada, ndipo walipoingia ndani ya nyumba na kugundua mtoto huyo amejeruhiwa vibaya na kuripoti tukio hilo uongozi wa kijiji.

Januari 14 mwaka huu tukio hilo lilifikishwa kituo cha polisi na alianza kusakwa kwa kushirikiana na wananchi hadi alipokamatwa.

“Bahati alifariki Januari 14 saa 12 jioni akiwa njiani kupelekwa hospitali kwenye matibabu kutokana na majeraha makubwa ya kuchomwa moto,” alisema Kamanda Malimi.

Alisema Jeshi la Polisi linaendelea kumhoji mtuhumiwa ili afikishwe mahakamani.

“Kumeanza kujitokeza wimbi la ukatili wa maisha dhidi ya watoto wadogo kutokana na ugomvi wa wazazi au wazazi kuchukua sheria mkononi dhidi ya watoto.

“Jambo hili halikubaliki na ni kinyume cha sheria, ni kosa kubwa la jinai, mzazi hana mamlaka kumpa mtoto adhabu hiyo, hivyo atakayebainika atakamatwa na tutahakikisha hatua kali zinachukuliwa dhidi yake,” alisema Kamanda Malimi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles