25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kisa Yanga Juuko akumbukwa Simba

ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

KITENDO cha Simba kupata matokeo ya sare mbele ya Yanga, kimewaibua wanachama wa klabu hiyo, ambao wameuomba uongozi wao kumrejesha beki, Juuko Murshid.

Simba juzi ililazimishwa sare ya mabao 2-2 na Yanga, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Simba ilitanguliwa kufunga mabao yake kupitia kwa Meddie Kagere kwa mkwaju wa penalti na Deo Kanda kabla ya Yanga kusawazisha kupitia kwa Mapinduzi Balama na Mohamed Issa ‘Banka’.

Simba iliachana na beki huyo raia wa Uganda, msimu uliopita kwa kile kilichodaiwa kutofiti katika mfumo wa kocha, Patrick Aussems.

Baada ya kuachwa na Wekundu hao wa Msimbazi, Juuko alijiunga na Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kwa mkataba wa miaka miwili, kabla ya kutemwa siku chache zilizopita.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu Mwenezi wa zamani wa Simba, Said Lubeya alisema kuwa, ameiangalia safu ya ulinzi ya Simba na kubaini Juuko alipaswa kuendelea kuichezea timu hiyo.

Juuko Murshid.

 “Pengo la Juuko limeonekana leo kiukweli hakukuwa na sababa ya kumuacha kwani alikuwa na kombinesheni nzuri na Pascal Wawa tofauti na ilivyo sasa anapocheza na Tairon Santos.

“Wawa hivi sasa umri  umekwenda, ili acheze vizuri lazima apangwe na mchezaji atakayemchangamsha kama kuna ulazima wa kumpanga, kwa kweli jana tulifungwa bao la kizembe sana hasa lile la pili.

“ Simba ina fedha lakini mpira ni mipango sio fedha kwani hazichezi, umefika wakati katika kipindi hiki cha dirisha wa dogo linalokwenda kufungwa kuhakikisha anarudishwa Juuko au mtu wa mfano wake,”alisema Lubeya na kuongeza.

“Kwa sababu Wawa anakata pumzi mapema, anahitahika mtu wa kumkimbiza lakini siyo huyo Santos ambaye anabebwa na jina la ubrazili tu.”

Katika hatua nyingine, Rais wa zamani wa klabu hiyo, Aden Rage, akizungumzia pambano hilo alisema: “ Simba haikuwa makini katika safu ya walinzi kwa sababu hakukuwa na maelewano mazuri kati ya Wawa na Santos.

“Wengi wana mlaumu Aishi Manula lakini kwangu naanzia katika safu ya ulinzi, Wawa amechoka hivi sasa na yule Mbrazil wao hakuna kitu, ni wao ndio waliosababisha Manula kuonekana mzembe.

“Kama ningekuwa mimi nipo madarakani, jambo la kuanza nalo ni beki, sijui kwanini waliwaondoa akina Juuko na kuwaacha hawa wengine.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles