29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Mkwasa: Simba tukutane Mapinduzi

ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

BAADA ya kuambulia sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Charles Mkwassa, amesema kiu yake ni kuhakikisha anawafunga Watani zao hao, na hilo atahakikisha linatimia endapo atakutana nao katika michuano ya Mapinduzi.

Yanga iliilazimisha Simba sare ya mabao 2-2, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA, baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mkwasa alisema walikuwa na kila sababu ya kupata ushindi dhidi ya Simba juzi kwani wapinzani wao hao walipoteana hasa kipindi cha pili.

“Simba waliidharau sana Yanga, kwa kuona wana kikosi kizuri huku wakiwa wamesahau mchezo ni mbinu unayoingia nayo, mwisho tumerudisha mabao wakiwa wameshatangulia na kupata sare.

“Matokeo haya hayajamaliza kiu niliyokuwa nayo kwa Simba, lakini sina shaka tunakwenda katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi, tutapambana tufikie hatua ya kukutana na Simba ili tuweze kuwafunga na kumaliza kelele zao,”alisema Mkwasa.

Michuano ya Mapinduzi ambayo ni maalum kwa ajili ya Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar itaanza kutumua vumbi leo, ambapo safari hii inaendeshwa kwa mtindo wa mtoano .

Yanga imepangwa kundi A, ikiwa pamoja na Azam, Mlandege na Jamhuri,  Simba ipo Kundi B sambamba na Mtibwa Sugar, Chipukizi na Mapinduzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles