31.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Maandamano makubwa yafanyika Iraq kumuaga Jenerali Soleimani

BAGHDAD, IRAQ

UMATI mkubwa watu umekusanyika katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad kushiriki maandamano ya mazishi ya kamanda wa jeshi la Iran Qasem Soleimani, aliyeuawa katika shambulio la angani lililotekelezwa na Marekani siku ya Ijumaa.

Soleimani alikuwa kiungo muhimu katika oparesheni ya Iran Mashariki ya kati na taifa hilo limeapa kulipiza kisasi mauaji yake.

Mkusanyiko huo wa mjini Baghdad ni mwanzo wa siku kadhaa za maombolezi ya Soleimani.

Makundi ya watu mjini Baghdad yalikuwa hapo kuomboleza kifo cha Abu Mahdi al-Muhandis, mmoja wa kamanda wa Iraq ambaye kundi lake la Kataib Hezbollah linaloungwa mkono na Iran pia aliuawa katika shambulio hilo.

Waandamanaji walianza kukusanyika mjini Baghdad mapema asubuhi jana wakipeperusha bendera ya Iraq na ya waasi wakiimba “kifo kwa Amerika”.

Waandamanaji walizunguka barabara za mji huo wakibeba mabango yaliyo na picha ya Soleimani huku wengine wakiwa na mabango yaliyo na picha ya kiongozi mkuu wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.

mwili ya raia huyo wa Iran aliyeuawa katika shambulio hilo ulisafirishwa jana jioni ambako siku tatu ya maombolezo imetangazwa kwa heshima ya jenerali.

Mazishi yake yatafanyika siku ya Jumanne nyumbani kwake Kerman eneo la kati la Iran.

Baadhi ya raia wa Iran walisherehekea taarifa za kuuawa kwa Soleimani mjini Baghdad.

Alilaumiwa kwa kupanga ghasia na kupinga maandamno ya amani ya kupigania demokrasia katika miezi ya hivi karibuni.

Televisheni ya taifa ya Iraq imetangaza mashambulio mengine ya angani nchini humo saa 24 baada ya kuuawa kwa Soleimani.

Vyanzo vya habari vya jeshi nchini Iraq vimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa watu sita wameuawa katika shambulio hilo jipya,ambalo lililenga msafara wa waasi wa Iraq asubuhi ya Jumamosi.

Msemaji wa jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani katika eneo hilo amesema hawakuhusika na shambulio hilo.

Marekani imesema kuwa wanajeshi 3,000 wa ziada watapelekwa mashariki ya kati kujibu hatua yoyote ya kulipiza kisasi.

Moja ya magari katika msafara wa Soleimani iiliwaka moto baada ya kushambuliwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa mjini Baghdad

Akizungumza na vyombo vya habari katika mgahawa wa Mar-a-Lago mjini Florida, Rais wa Marekani, Donald Trump alisema katika shambulio la siku ya Ijumaa Jeshi la Marekani katika opareshi stadi ilifanikiwa kumuua gaidi nambari moja duniani, Qassem Soleimani.

Trump alisema Soleimani alikuwa “anapanga kushambulia wanadiplomasia na maofisa wa kijeshi wa Marekani lakini walifanikiwa kumpata kabla hajatekeleza mpango wake na kumuangamiza.

Hata hivyo maafisa wa utawala wa Trump hawakutoa taarifa zaidi kuhusiana na shambulio hilo na kile kilichowafanya kuchukua hatua ya kumuua ghafla Soleimani.

Marais wa zamani wa Marekani Barack Obama na George Bush wamepinga hofu kuwa shambulio dhidi ya jenerali huyo lilikuwa hatari.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetoa onyo kwa raia wake baada ya shambulio hilo kuondoka Iraq mara moja kupitia njia yoyote inayowezekana.

MFAHAMU Qasem Soleimani

Qasem Soleimani anasadikiwa kuwa mtu wa pili maarufu katika Jamhuri ya Kiislam ya Iran baada ya kiongozi wa kidini Ayatollah Ali Khamanei.

Kama kiongozi wa kikosi maalum cha jeshi la ulinzi wa Iran nje ya nchi kinachofahamika kama Quds, Soleimani alikuwa kiungo muhimu katika kampeni zote za kijeshi za Iran kwenye mataifa ya kigeni, na kuwa waziri wake wa Mambo ya nje linapokuja suala la vita na amani.

Inasadikiwa kwamba alikuwa mshirika wa rais Bashar al-Assad katika vita dhidi ya waasi nchini Syria, kubuniwa kwa vikosi vya angani vinavyoungwa mkono na Iraq, mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic State, na mengine mengi.

Akiwa mkuu wa kikosi cha Quds Soleimani alisimamia operesheni za kijeshi nje ya Iran katika hatua ambayo ilimfanya kuingia uhasama na Marekani wakati wa vita vya Iraq

Akionekana kuwa mfadhili wa makundi ya wanamgambo wa kishia.

Marekani iliilaumu kikosi cha Quds kwa shambulio la Karbala lililosababisha vifo vya wanajeshi wake watano pamoja na kutoa mafunzo kwa watengenezaji mabomu yaliotumika kuvilenga vikosi vyake.

Tangu mwaka 2013, Ofisa wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA), John Maguire, aliliambia gazeti la New York kwamba Soleimani “alikuwa mtu mmoja mwenye uwezo mkubwa mashariki ya kati”.

Januari 3 Pentagon ilitangaza kuwa ilimuua Jenerali huyo kwa agizo la Rais Donald Trump.

Mauaji yake yamesababisha kuongezeka kwa uhasama mkali kati ya Marekani na Iran pamoja na makundi yanayoungwa mkono na Iran- nchini Iraq.

WASIFU WAKE

Soleimani anaamika kulelewa katika familia masikini na hakupata masomo rasmi.

Amepanda katika ngazi ya kikosi cha ulinzi wa Iran Revolutionary Guards – kupitia kikosi chake cha Quds ambacho kinaripoti moja kwa moja kwa kiongozi mkuu wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, na ilipewa hadhi ya shujaa wa kitaifa.

Tangu mwaka 1998, Meja Jenerali Qasem Soleimani ameongoza vikosi vya Quds nchini Iran- kitengo maalum cha jeshi la Iran (Revolutionary Guards) ambacho huendesha opareshani zake nje ya nchi.

Alikuwa kiungo muhimu katika mapambano ya kimkakati mashariki ya kati kupitia vikosi vya Quds, ambavyo vinaendesha oparesheni yake kwa ushirikiano na jeshi la ulinzi la Iran.

Jina lake lilianza kuwa maarufu alipopewa nafasi ya kuongoza kikosi cha Quds na kujenga ushirikiano wa karibu na kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Khamenei kiasi wakati mmoja kiongozi huyo alishiriki na kufungua dhifa ya harusi ya binti ya Jenerali Soleimani.

Meja jenerali Qasem Soleimani, na vikosi vyake vinafanya kazi chini ya kiongozi mkuu wa kidini, Ayatollah Ali Khamanei, badala ya kufuata muundo wa kawaida wa kijeshi wa Iran.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alitaja jeshi la ulinzi la Iran Revolutionary Guards na washirika wake vikosi vua Kikurdi kama shirika la kigeni la ugaidi mwezi April mwaka jana.

Jenerali Qasem Soleimani hakuwa anajulikana na wengi nchini Iran hadi mwaka 2003 wakati Marekani ilipoivamia kijeshi Iraq.

Umashuhuri wake uliimarika hatua ambayo ilifanya maofisa kadhaa wa Marekani kutoa wito wa kuuliwa kwake.

Muongo mmoja na nusu baadae Soleimani alifikia kuwa kamanda maarufu wa vita nchini Iran kiasi akipuuza miito ya umma kumtaka aingie kwenye siasa.

Baada ya Marekani kuivamia Iraq kijeshi mwaka 2003 alianza kutoa amri kwa makundi ya waasi kushambulia kambi ya kijeshi ya Marekani, na kuwaua mamia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles