25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mtaalamu atoa somo la mlo kamili

Na AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM

 MTAALAMU na mtafiti wa lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Abela Twin’omujuni, amewashauri wanaokula mbogamboga na matunda pekee wakifikiri ni mlo kamili (balance diet) waache, badala yake wale vyakula vyote kutoka makundi matano kwa vipimo.

Akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalumu jana Dar es Salaam, alisema kuna baadhi ya watu wanaamini kuwa ‘balance diet’ ni ulaji wa matunda na mbogamboga, huku wengi  wakipunguza milo kwa siku kitu ambacho si sahihi

“Ukweli ni kwamba unapozungumzia ‘balance diet’ unazungumzia mlo kamili. Hii inatoka katika makundi matano ya vyakula, mlo hauwezi kuwa kamili kama hauli vyakula kutoka makundi yote. Mtu anayekula mbogamboga pekee au matunda hiyo si ‘balance diet’.

“Ili uitwe mlo kamili kuna vigezo ya makundi ya chakula, kiwango kinachostahili mtu ale, matayarisho yake na kingine ulaji wa mtu, mwili wake uko katika kiwango sahihi mtu anapokula chakula, kwahiyo kuna watu hawaelewi wanafikiri ukila matunda tu au mbogamboga za majani ni ‘balance diet’, watu wabadilike,” alisema Abela. 

Alibainisha kuwa mtu anatakiwa ale chakula kulingana na aina ya kazi anayofanya kwani kiwango cha kazi ndicho kinaratibu kiwango cha matumizi ya chakula mwilini.

“Tunaposema kuwa kula ‘balance diet’ unatakiwa ule vyakula vyote kutoka katika viwango sahihi, hii inatofautiana na mazingira na kazi anayofanya. Mfano mtu anayefanya kazi nzito ni tofauti na anayekaa ofisini.

“Kwahiyo ulaji hauwezi kuwa sawa, watu wanaofanya kazi za nguvu chakula kinatumika, lakini kama unakula chakula kingi na unakaa tu chakula hakitumiki hivyo kinabaki mwilini, kuna watu wengi wanakuwa hawali milo mitatu kwa siku wakifikiria ni ‘balance diet’, hii pia si sahihi, ni bora mtu ale milo yote kwa kiwango na uwe kamili,” alieleza.

Alisema kila makundi ya chakula katika mwili yana kazi zake, kwahiyo ili mtu aweze kutengeneza afya nzuri, ni bora akazingatia mlo kamili na pia kufanya mazoezi.

“Kundi la mbogamboga zinatusaidia kupata vitamini C, watu wamezoea mbogamboga ni zile za majani, lakini kuna karoti, nyanya, bamia, nyanya chungu na nyingi. 

“Kundi la kwanza la mlo ni nafaka, mizizi na ndizi, hili linaitwa wanga. Kundi la pili ni vyakula vyenye asili ya nyama na kunde ambalo linaitwa protini. Kundi la tatu ni mbogamboga za kijani na ambazo si za kijani ambalo linaitwa vitamin. Kundi la nne ni matunda linaitwa vitamin na madini na kuna kundi la vyakula vyenye mafuta.

“Mbogamboga na matunda huwa zinatunzwa mwilini, hivyo inaweka akiba ya chakula. Tukija kwenye mbogamboga, mtu anatakiwa ale viganja viwili vilivyojaa vya mboga kwa siku na matunda ya aina tofautitofauti kila moja kipande,” alisisitiza Abela. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles