30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanaume aliyeweka sheria kali dhidi ya uzinzi yamjeruhi

JAKARTA, INDONESIA

MWANAUME mmoja nchini Indonesia aliyeweka sheria dhidi ya uzinzi naye ameshikwa na kosa la kutembea na mke wa mtu.

Mukhlis bin Muhammad kutoka baraza la Aceh Ulema amekuwa kiongozi wa kwanza kupigwa viboko 28 kwa kosa la uzinzi mbele ya kadamnasi.

Mwanamke ambaye alikuwa na mahusiano naye alichapwa viboko 23.

Mukhlis anatokea katika mji pekee nchini Indonesia ambao unafuata sheria za kiislamu , zinazojulikana kama sharia.

Mbali na sheria hizo kuwaadhibu wazinzi, pia wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wanaadhibiwa katika umati wa watu kwa kupigwa viboko.

Husaini Wahab ambaye ni Meya msaidizi wa eneo hilo la Aceh Besar aliiambia BBC kuwa; “Hii ni sheria ya Mungu. Mtu yeyote anayekosea lazima aadhibiwe na sheria hizo,”

Wapenzi hao walikamatwa na maofisa mwezi Septemba mwaka huu wakiwa katika gari ambalo lilikuwa limeegeshwa karibu na ufukwe wa kitalii.

Husaini alisema kuwa wapenzi hao walichapwa siku ya alhamisi wiki hii.

Mwanaume huyo aliyekamatwa ugoni ni kiongozi pia wa dini ya ya kiislamu.

Yeye ni kiongozi wa kwanza kupigwa katika kadamnasi kwa mujibu wa sharia iliyowekwa katika mji huo na kuanza kufanya kazi tangu mwaka 2005.

Ofisa huyo ameshauri serikali ya mtaa na watunzi wa sheria ambao wanatekeleza sheria hiyo kufanya mabadiliko.

Aceh ilianzisha sheria ngumu za Kiislamu kwa zaidi ya muongo mmoja ili watu wapate haki zao.

Sheria dhidi ya wapenzi wa jinsia moja ilianzishwa mwaka 2014 na kuanza kufanya kazi mwaka uliofuata.

Kuwa na wapenzi wengi, kucheza kamali na matumizi ya pombe ni kinyume na sheria katika sharia ya kiislamu.

Mwaka 2017, wanaume wawili walipigwa fimbo 83 huko Aceh baada ya kukutwa wakifanya mapenzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles