Wanajeshi 53 wauawa Mali

0
852

BAMAKO, MALI

IDADI ya wanajeshi wa Mali waliouawa katika shambulizi la kigaidi imefikia 53. Jeshi la Mali limesema katika tovuti yake kwamba idadi hiyo imeongezeka kutoka 15 ya awali.

 Shambulizi hilo limetokea kwenye kambi ya jeshi kwenye eneo la Indelimane, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Serikali ya Mali imelaani vikali shambulizi hilo ambalo ni pigo jingine kwa jeshi la Mali.

Mwishoni mwa mwezi Septemba, jeshi la Mali lilishambuliwa tena, ambapo wanajeshi 38 waliauwa katika mashambulizi ya kupangwa kwenye kambi mbili za jeshi katikati mwa Mali, licha ya uwepo wa majeshi ya Ufaransa na vikosi vingine vya kimataifa.

Wapiganaji wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda pamoja na makundi ya kigaidi yenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS yamekuwa yakifanya mashambulizi kwenye ukanda wa Sahel na kuvuruga utulivu kwenye maeneo ya Niger na Burkina Faso.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here