30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

IGP Sirro ataka kuacha kugeuzwa wapiga debe, kutumika

Na SHEILA KATIKULA-MWANZA

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro  amewataka vijana  kuacha kufanya kazi ya  kupiga debe badala yake kutafuta shughuli nyingine sambamba kujiepusha kutumiwa na makundi ya watu kwa maslahi yao.

Rai hiyo ilitolewa juzi wakati akizungumza na wamachinga wa jijini Mwanza.

Alisema inasikitisha kuona kijana mwenye nguvu anajishughulisha na kazi ya kupiga bede ambayo niya kipindi cha muda mfupi  ambayo hawezi kuifanya baada ya umri kusogea.

Kutokana na hilo ameshauri vijana kubuni kazi  nyingine za kujiingizia kipato.

“Huwa ninasikitika sana nikisikia kijana mwenye nguvu ambaye anaweza kuchangamkia fursa mbalimbali anasema anapiga debe hivi hii kazi unaweza kuifanya hadi uzeeni?…mtoto wako anaenda shule anakukuta unafanya kazi hii atajisikiaje inasikitisha.

“Nawaomba mnaofanya kazi hii muache mara moja  japo mnapata fedha ila tafuteni kazi ambayo utaifanya hadi  uzeeni.

Aliongeza kuwa kila machinga na wafanyabiashara  wanapaswa kulipa kodi ya  mapato  kwa wakati kwani mambo ya kukimbizana yamepitwa na wakati.

Pamoja na hayo amewataka vijana kuacha kutumiwa na makundi ya watu kufanya uhalifu kwani kufanya hivyo ni kosa na ukibaika utawajibika

“Msikubali kutumiwa  na vikundi vya watu kufanya uhalifu kwani tukikugundua utawajibika mwenyewe ni bora umwambie huwezi kujihusisha na mambo hayo, nawaomba mchague viongozi wanaofaa wa serikali za mtaa uchaguzi umekalibia msifanye fujo.

” Kila mtu anaona uelekeo tunapokwenda msifanye fujo  kwani ukichagua kiongozi wakati wa fujo hautamchagua unaye mtaka ila ukiwa na amani utamchagua mzuri nitajisikia vibaya mkienda tofauti na maelekezo yangu ,”alisema Sirro.

Naye Mhasibu wa umoja wa machinga mkoani hapa , Yohana Chacha akisoma risala alisema tangu mwaka 2014 umoja huo uliposajiliwa  umesambaa mikoa 16  nchi lengo ni kuhakikisha  kila mtu anafanya kazi halali ya kujiingizia kipato  na kujiepusha na uhalifu.

“Tunashirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha kila machinga anatii sheria bila shuruti kwani jamii inahitaji kukumbushwa nadhani kila mtu anakumbuka huko nyuma machinga walikuwa wanawarusha mawe na kuchoma mataili ila sasa yamekwisha baada ya kupewa elimu na kutii.

Hata hivyo aliiomba Serikali kupunguza utitiri wa viongozi wa vikundi visivyo rasmi  vya watu binafsi kwani machinga siyo sehemu ya siasa.

Alismea vikundi hivyo  vyote hufanya kazi moja tofauti ni majina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles