28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa atangaza kihama watendaji wanaoomba wawekezaji rushwa

Gustaph Haule -Pwani

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesema Serikali inaendelea kudhibiti vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watendaji ili kutoa nafasi nzuri kwa wawekezaji kufanya shughuli zao.

Majaliwa ,alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wawekezaji, wakuu wa taasisi za kibenki na wataalamu mbalimbali katika ufunguzi wa kongamano la wawekezaji linalofanyika Mkoa wa Pwani.

Aliwaekeza wawekezaji hao endapo watakuwa wanaombwa rushwa na mtu au taasisi yoyote, watoe taarifa mapema ili watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo wachukuliwe hatua.

Alisema Serikali inadhamira ya a kukuza uchumi kupitia viwanda na kuendelea kuwavutia wawekezaji lakini wapo baadhi ya watumishi na watendaji wa taasisi mbalimbali wanaoomba kwa wawekezaji hao.

Alisema, tabia hiyo ni mbaya na inakwamisha juhudi za wawekezaji na hata kupoteza mapato ya taifa yanayotokana na uwekezaji.

“Serikali inaendelea kudhibiti vitendo vya rushwa hivyo wawekezaji mnaokuja msipate hofu, nawaomba mwekezaji yeyote atakayeombwa rushwa atoe taarifa mapema na Serikali itamchukulia hatua mhusika haraka ili hiwe fundisho kwa wengine,”alisema Majaliwa.

Majaliwa, alisema Tanzania inauchumi imara ambapo miaka minne iliyopita, pato limekuwa kwa asilimia 7 na mwenendo huo unaifanya Tanzania kuwa kati nchi ya tano Afrika ambazo uchumi wake unakuwa haraka.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo, alisema kufanyika kwa kongamano hilo limetokana na agizo lake alilotoa Juni 18 mjini Dodoma .

Ndikilo alisema lengo la kongamano hilo ni kutangaza fursa za uwekezaji na kuvutia wawekezaji wengi zaidi kwenda mkoani Pwani, kuainisha muongozo wa uwekezaji na kutafuta masoko kwa ajili ya kutangaza bidhaa zinazozalishwa na wamiliki wa viwanda waliopo mkoa wa Pwani.

Alisema mkoa huo mpaka sasa una viwanda 1,192  vikiwemo vikubwa na vidogo 140 na kwamba umekusudia kuongezea msukumo zaidi katika viwanda na hata katika ufugaji, kilimo, uvuvi na ufugaji ambapo ameomba Majaliwa kuufanya Mkoa wa Pwani kuwa ukanda wa Viwanda.

Ndikilo, alisema bado kuna changamoto za ukosefu wa miundombinu mizuri ya barabara, maji, umeme, urasimu wa kupata vibali, gharama kubwa za ardhi na mgongano wa taasisi huku akisema baadhi ya changamoto zinafanyiwa kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles