Amina Omari, Korogwe
Serikali imegawa hati 250 za kimila za matumizi bora ya ardhi kwa wilaya ya Korogwe ili kudhibiti uharibifu wa vyanzo vya maji.
Akikabidhi hati hizo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mwanasha Tumbo amesema kuwa ugawaji wa hati hizo umelenga katika kuhakikisha wanadhibiti uharibifu wa mazingira pamoja na kupunguza migogoro ya ardhi.
“Maji ni rasilimali muhimu hivyo ni lazima tuweke mipango endelevu ya kuhakikisha rasilimali hiyo inadumu kwa muda mrefu,” amesema.
Aidha mwakilishi mkazi wa UNDP Christine Musisi amesema kuwa uwepo wa hati hizo utaweza kusaidia kumaliza migogoro ya ardhi pamoja na kurasimisha makazi Bora kwa wananchi.