31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania kuwezeshwa fursa SADC

Eliya Mbonea, Arusha

Kamati ya Habari, Matangazo, Burudani na Utamaduni imejipanga kuratibu na kutoa taarifa zitakazowezesha Watanzania kufahamu fursa na faida zilizopo Jumuiya ya SADC kupitia mikutano mbalimbali ya kisekta zaidi ya 30 inayoendelea.

Kauli hiyo imetolewa  na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Agness Kayola leo Oktoba 17, mjini Arusha wakati wa semina kwa wanahabari wanaotarajiwa kuripoti mkutano wa Mawaziri wa Mazingira, Maliasili na Utalii wa SADC.

Kupitia semina hiyo mada mbalimbali ziliwasilishwa kwa wanahabari hao ili kuwajengea uelewa wa SADC na maendeleo ya Utalii, mazingira, misitu na sekta ya Wanyamapori.

Akifungua semina hiyo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk Aloyce Nzuki amesema nchi 16 mwachama wa SADC zinatarajiwa kushiriki ambapo ameyataja dhumuni la mkutano huo ni kuangalia hali ya mwenendo wa mazingira kwa nchi hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles