26.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

RITA yahamasisha uandikaji wosia kwa wakazi Dodoma

MWANDISHI WETU-DODOMA

WAKALA  wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umetoa rai kwa wakazi wa Dodoma kuchangamkia fursa ya kuandika na kutunza wosia inayotolewa na wakala huo  mkoani hapo.

Akizungumza jana na MTANZANIA Ofisa Habari wa RITA,  Jafari Malema alisema Wakala ulianzisha huduma hiyo mwaka 2008 na muda wote imekuwa ikitolewa katika Ofisi ya Makao Makuu jijini Dar es Salaam lakini kutokana na Dodoma kuwa makao makuu ya Serikali kumekuwa na ongezeko la watu na wakala umeanza rasmi kutoa huduma hiyo.

Alisema huduma zote zinazotolewa na wakala ikiwa pamoja na wosia kwa sasa zinapatikana katika Ofisi ya RITA iliyopo katika Jengo la Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ghorofa ya pili hivyo wanachi wanatakiwa kuchangamkia na kupata huduma mbalimbali katika ofisi hiyo.

“Wosia ni kauli inayotolewa na mtu wakati wa uhai wake kwa hiari yake kuonyesha nia yake jinsi gani angependa mali yake igawanywe baada ya kufa kwake pia  husaidia kuepusha migogoro baina ya wanafamilia ambayo mara nyingi husababisha warithi halali hasa wake wa marehemu na watoto kukosa haki zao kama warithi halali.

“RITA inatoa huduma ya kuandika Wosia kwa kutumia wanasheria waliobobea katika masuala ya mirathi na Wosia na mwananchi akifika katika Ofisi ya Wakala jijini Dodoma ataweza kufanya majadiliano, kupewa ushauri na kuelezwa mambo yote muhimu kabla ya kuandika wosia ambao tunawahahikishia utafuata matakwa yote ya kisheria,” alisema  Malema.

Akizungumza kuhusu mwamko wa wananchi kuandika wosia alisema hali sio ya kuridhisha kwani bado wengi wanasita kuchukua hatua wakiamini kuandika Wosia ni uchuro  na kwamba kuandika ni kujitabiria kifo dhana ambayo alieleza kuwa ni  potofu kwani wapo wananchi walioandika wosia tangu huduma hiyo kuanzishwa  na wakala na hawajafariki.

Alisema  mpaka sasa RITA imeandika wosia 611 ambapo kati ya hizo 26 zilishafungwa.

“Vilevile kuanza kutolewa huduma hii katika Ofisi ya Mkoa wa Dodoma na maeneo mengine nchini itaongeza idadi ya wananchi wanapata huduma hii kwani huduma itakuwa imesogezwa karibu na maeneo wanayoishi,” alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles