30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mchango wa sekta isiyo rasmi ni mkubwa- ILO

Mwandishi wetu -Dar es salaam

MWAKILISHI wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini, Wellington Chibebe amesema sekta isiyo rasmi ni sekta muhimu kwa mustakabala wa ustawi wa uchumi wa Bara la Afrika.

Hayo aliyasema mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati wa kupokea taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa Utafiti wa Sekta Isiyo Rasmi wa Mwaka 2019 unaoendelea mkoani Dar es Salaam hivi sasa.

Chibebe alieleza kuwa sekta hiyo inachangia sehemu kuwa ya uchumi wa nchi nyingi barani Afrika.

“Katika nchi nyingi barani Afrika sekta isiyo rasmi inachukua karibu asilimia 85 ya uchumi na katika nchi zilizo chini ya jangwa la Sahara ni zaidi ya kiwango hicho” alisema kabla ya kutembelea eneo la Kipunguni kuangalia utekelezaji wa utafiti huo.

Alitoa mfano kuwa akiwa nchini Kenya Agosti, 2019 walielezwa kuwa sekta isiyo rasmi nchini humo inachangia asilimia 34 ya pato la taifa hivyo ni sekta ambayo inapaswa kuendelezwa kwa kuimarishwa ili iweze kuboresha ustawi wa washiriki wake na kuinua pato la taifa.     

Aliongeza kuwa suala la kuifanya sekta hiyo kuwa rasmi kwa shirika lake ni jambo la kipaumbele hasa ukizingatia kuwa sekta hiyo imeshikwa na vijana na wanawake makundi ambayo ni sehemu kubwa ya wakazi wa Afrika hivyo hayawezi kuachwa nyuma.

Chibebe ambaye anawakilisha Shirika hilo pia katika nchi za Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda alieleza kuwa shirika lake lina uzoefu mkubwa wa sekta hiyo ambapo kwa mara ya kwanza lilifanya kazi nchini Kenya mwaka 1973.

“Tunafurahi kufanya kazi na serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS),  ambao wanaendesha utafiti huu na sisi tunawasaidia utaalamu pamoja kuwapatia vifaa vya kisasa vinatakavyotumia kutekeleza utafiti huu” Alieleza.

Mkurugenzi huyo wa ILO alibainisha kuwa matokeo ya utafiti huo yatasaidia sana serikali na wadau katika kuangalia namna ya kuikuza sekta hiyo na kuitoa ilipo na kuifikisha katika nafasi inayostahiki.

Mapema akieleza lengo la Utafiti huo, Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Makazi, Ruth Minja alieleza kuwa utafiti huu umelenga kubaini ni kwa kiasi gani sekta hii imekuwa ikichangia katika pato la taifa.

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema kuwa ziara hiyo kwa viongozi watataka kufahamu hatua ambazo wajasiriamali wamekuwa wakichukua kukukabiliana na changamoto zinazowakabili pamoja kupata maoni yao kuhusu ni maeneo gani wanadhani serikali inaweza kuwasaidia ili sekta hiyo iweze kukua na wao kuongeza kipati chao na kuongeza mchango wake katika pato la taifa.

“Tunatarajia matokeo ya utafiti huu yatatangazwa mwezi Disemba mwaka huu na baada ya hapo tutakuwa tumepata msingi mzuri wa namna ya shughuli katika sekta hii zinavyoendeshwa hapa nchini,” alisema

Alibanisha kuwa wameuchagua Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa ni kitovu cha biashara ambapo wananchi wengi mkoani humo wamejiajiri kwenye sekta hiyo na kwamba matokeo na uzoefu utakaopatikana hapa utatumika katika mikoa mingine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles