26.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

AAR yatoa ushauri nasaha, kupima afya mawakala

Mwandishi wetu -Dar es salaam

KAMPUNI inayoongoza kwa kutoa bima ya afya Tanzania, AAR, imewapima na kuwapa ushauri nasaha mawakala wao Dar es Salaam ikiwa kama njia kuimarisha uhusiano wao.

Vipimo vilivyotolewa mwishoni mwa wiki ni pamoja na kipimo cha sukari, shinikizo la damu, uwiano wa uzito na urefu huku wakiwapatia ushauri nasihi wa ustawi kama jinsi ya kukabiliana na msongo wa mawazo, lishe bora, utumiaji sahihi wa fedha na maradhi ya homa ya ini.

Meneja Masoko na Mauzo wa AAR Insurance Tanzania, Tabia Masudi, alisema wamebaini mawakala wao wana uhitaji wa elimu juu ya kutunza afya zao za mwili na akili kwa uboreshaji bora wa maisha yao na biashara.

“Tukiwa kama wadau wakuu wa afya nchini, tunaamini ni jukumu letu kuwapa wadau wetu taarifa sahihi na msaada wa matibabu ambao utanufaisha afya zao za mwili na akili.

“Tunatambua nafasi kubwa ya mawakala katika ukuaji wa bima ya AAR, hivyo tunalo jukumu la kujali afya zao na ndiyo maana leo tumetumia nusu ya siku kufanya zoezi hili sio tu katika kuwahimiza kuangalia afya zao mara kwa mara, lakini pia kuwapa mwongozo juu ya afya ya akili,” alisema Tabia.

Mmoja wa mawakala ambaye alipokea ushauri nasihi na kupata vipimo kutoka kampuni hiyo, Dk. Sara Nyero kutoka ARIS, alitoa shukrani huku akiwapongeza kwa huduma zao za ustawi wa mfanyakazi.

“Kwa niaba ya mawakala wenzangu, ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Kampuni ya bima ya AAR kwa ushauri nasihi na huduma zote za afya walizotupatia, tumejifunza vitu vingi sana ambavyo vitatusaidia sana katika kulinda afya zetu za mwili na akili.

“Ningependa pia kuwapongeza kwa hatua hii ya kuonyesha kutujali sisi kama mawakalo wao, hii itasaidia kuimarisha uhusiano wetu na AAR na kutufanya kuwa mabalozi wazuri wa huduma yao ya ustawi wa mfanyakazi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles