27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Callum Hudson-Odoi alikuwa muokota mipira Chelsea sasa staa wao

 BADI MCHOMOLO NA MITANDAO

NDOTO za wachezaji kufika mbali katika mchezo wa soka wengi wao zinaanzia wakiwa na umri mdogo kutokana na kuwaona mastaa mbalimbali wakifanya mwakubwa duniani.

Wengine wanakuwa hawana ndoto hizo, lakini kutokana na mazingira yanayowazunguka yanawafanya kutumia muda mwingi kuwa karibu na mchezo huo na baadae kujikuta wakicheza soka.

CALLUM Hudson-Odoi ni nyota anayekuja kwa kasi katika klabu ya Chelsea huku akiwa na umri wa miaka 18 tayari ameanza kuonesha maisha yake ya baadae katika mchezo huo.

Mchezaji huyo mwenye urefu wa futi tano na nchi 10, alipandishwa kwenye kikosi cha kwanza tangu mwaka 2017, akitokea timu ya Chelsea ya vijana, lakini alikuwa hana nafasi ya kudumu chini ya makocha walioondoka ikiwa pamoja na Maurizio Sarri, lakini msimu huu anaweza kupata nafasi chini ya kocha mpya Frank Lampard.

Anaweza kupata nafasi kubwa kutokana na timu hiyo kutofanya usajili msimu huu baada ya kufungiwa na FIFA, huku baadhi ya wachezaji kama vile Eden Hazard akiondoka na kujiunga na Real Madrid, hivyo hali hiyo itamfanya mchezaji huyo kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Mbali na kubaguliwa na mashabiki, lakini mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji ambao watakuwa wanaumia kwa kuona timu hiyo ikipata matokeo mabaya kwa kuwa amekulia kwenye timu hiyo tangu akiwa na umri wa miaka saba.

Kabla ya kupandishwa kwenye kikosi cha wakubwa akitokea timu ya vijana, alikuwa ni muokota mipira kwenye uwanja wa Stamford Bridge tangu akiwa na miaka saba mwaka 2007 hadi 2017 alipopandishwa.

Ndoto zake kubwa zilikuwa siku moja kuja kuisaidia Chelsea kutwaa mataji na kushinda michezo mbalimbali endapo atapata nafasi ya kuvaa jezi ya timu hiyo.

Mwaka 2014 akiwa na umri wa miaka 13, alikuwa na furaha kubwa baada ya kushikwa mikono na aliyekuwa staa wa timu hiyo Samuel Eto’o wakati Chelsea inashinda mabao 3-1 dhidi ya Manchester United.

Mabao hayo yote ya Chelsea yaliwekwa wavuni na Eto’o, hivyo mchezaji huyo baada ya kufunga bao la pili alikimbia hadi alipo muokota mipira huyo na kumshika mikono huku akiwa amekaa chini, jambo ambalo lilikuwa ni kumbukumbu katika maisha yake.

Kitendo cha Eto’o kumshika kijana huyo mkono kimemfanya awe hapo alipo leo kwa kuwa ilikuwa ni sehemu ya furaha kushikana mkono na staa, hivyo akili zake zote zikawa kwenye soka ili na yeye siku moja aje kuwa staa.

“Nilikuwa na ndoto za kuja kuwa staa, nimekuwa nikimuangalia sana Samuel Eto’o, natamani siku moja kuja kuwa mfalme wa soka kama ilivyo yeye na ninaamini ninaweza kufanya hivyo kwa kuwa bado ninapambana kwa ajili hiyo.

“Soka sasa ni sehemu ya maisha yangu, nimeanza kuupenda mpira tangu nikiwa na umri mdogo, nimekulia ndani ya Chelsea, hivyo nina kazi kubwa ya kuifanya ili kutimiza ndoto za timu kwa kuwa wameanza kuniamini kunipa nafasi katika kikosi cha kwanza,” alisema mchezaji huyo.

Lengo lake kubwa ni kuja kuacha historia katika klabu hiyo kama alivyoacha Eto’o, anaamini inawezekana kutokana na matumaini anayopewa na kocha wake mpya Lampard.

Mipango ya Lamprd ni kuwatumia wachezaji wengi vijana wenye damu changa ambao watakuja kuwa tegemeo kubwa kwa timu hiyo.

Kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili nchini England wakati huu wa kiangazi, Hudson-Odoi alikuwa mmoja kati ya wachezaji wanaowindwa na mabingwa wa Ligi Kuu nchini Ujerumani, Bayern Munich, ambao walikuwa tayari kuvunja benki yao kwa ajili ya kutaka kuinasa saini ya mchezaji huyo, lakini Lampard alikataa kumuacha aondoke huku akimuhakikishia namba kwenye kikosi chake.

Lampard amewataka mashabiki wa timu hiyo kuendelea kumpa sapoti kubwa kwa kuwa anaamini atakuwa na msaada mkubwa kwenye kikosi hicho mbali na kushindwa kuisaidia timu kwenye fainali ya Europa Super Cup.

Mwishoni mwa wiki iliopita Chelsea ilifanikiwa kuanza na ushindi katika mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Norwich City kwa mabao 3-1, ambapo mabao hayo yamefungwa na wachezaji chipukizi Tammy Abraham mwenye umri wa miaka 21 aliyefunga mabao mawili huku bao moja likifungwa na Mason Mount.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles