25.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Chilunda atuliza presha Azam

MOHAMED KASSARA – DAR ES SALAAM

MSHAMBULAJI wa Azam FC, Shaaban Chilunda, amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo wanaodhani amechemsha kucheza soka la kulipwa Ulaya, akiwataka kusubiri kuona moto atakaouwasha Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa msimu ujao.

Chilunda alijiunga na klabu ya CD Tenerife inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania kwa mkataba wa miaka miwili, akitokea Azam, Agosti mwaka jana.

Januari mwaka huu, timu hiyo ilimtoa kwa mkopo kwenda klabu ya CD Izarra inayoshiriki Ligi Daraja Pili nchini humo, hata hivyo mshambuliaji huyo alirudi Azam baada ya timu hizo kutofikia makubaliano kuhusu kumbakiza.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Chilunda alisema amejipanga upya kuhakikisha anaonyesha kiwango cha juu kwenye Ligi Kuu Bara na michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ili kusaka tiketi kwenda tena nje.

“Nimejipanga kuanza upya, kujipanga na safari ya kucheza Ulaya, bado nina umri wa kutosha kupanga mipango na naamini kwa uwezo wa Mungu, nitafanikiwa. Kwa sasa naelekeza nguvu kuhakikisha nacheza katika kiwango bora katika michuano ya ligi na kimataifa. “Wanaodhani labda nimeshuka kiwango baada ya kurejea, wasubiri kuniona kwenye ligi, sitakuwa na cha kuongea sana kwa kuwa naamini bado nipo katika kiwango cha juu, wataona pia kama Ulaya nilikuwa najifunza au nilienda tu kuzuga, najua hii nafasi nyingine ya kucheza nje nitadhibitisha hilo uwanjani,” alisema Chilunda.  

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles