25.7 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa: Wakulima changamkieni fursa CRDB

Mwandishi wetu, Simiyu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka wakulima nchini kuchangamkia fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB kupitia akaunti ya “FahariKilimo” ambayo ni maalum kwa ajili ya wakulima.

Akizungumza wakati wa kilele cha maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nane Nane) yaliyofanyika kitaifa mkoani Simiyu, amesema akaunti hiyo ya ambayo imeambatana na fursa nyingine za uwezeshaji ikiwamo mikopo kwa wakulima itasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha mnyororo wa thamani wa kilimo nchini.

“Serikali inaridhishwa sana na jitihada kubwa zinazofanywa na benki hii ya CRDB katika kuboresha sekta ya kilimo nchini, ubunifu huu wa huduma na bidhaa mnazozitoa kwa wakulima unaambatana na dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa kati wa viwanda ukizingatia malighafi ya viwanda vyetu inapatikana katika sekta hii mama ya kilimo,” amesema.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimuelekeza jambo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati alipotembelea Banda la Benki ya CRDB, katika kilele cha Maonyesho hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela, amesema akaunti hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa benki hiyo kuwahudumia wakulima kwa ukaribu zaidi kwa kuzingatia mahitaji yao.

 “Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba nikujulishe kuwa akaunti hii ya FahariKilimo hufunguliwa bure kabisa na hakuna gharama zozote za uendeshaji wa akaunti kwa mkulima, tukilenga kumpa mkulima unafuu wa kupokea malipo yake baada ya kuuza mazao,” amesema Nsekela.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles