Waziri Mkuu aitaka JKT kutoa elimu ya kilimo bora kwa wakulima

0
659
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia viatu ambavyo vinazalishwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wakati alipotembelea eneo la jeshi hilo kwenye maonesho ya sikuu ya wakulima kitaifa (Nanenane), ambayo yanahitimishwa leo katika viwanja vya Nyakabidi mkoani Simiyu.

Derick Milton, Simiyu

Waziri Mkuu kassimu Majaliwa, amelitaka jeshi la kujenga Taifa (JKT), kuendelea kuwepo katika eneo la maonesho ya Nanenane Nyakabindi Mkoani Simiyu, ili kuweza kutoka elimu ya kilimo bora cha mazao mbalimbali kwa wakulima wa mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara.

Amesema hayo leo Alhamisi Agosti 8, wakati alipotembelea eneo la jeshi hilo kukagua shughuli zinazofanywa za kilimo, ujasiriamali pamoja na uvuvi kwenye maonesho ya sikuu ya wakulima kitaifa.

Aidha amelitaka jeshi hilo kuhakikisha linaenda maeneo ya vijijini kuwafuata wakulima na kuwapa elimu ya kulima kwa ufanisi kwa kufuata kanuni bora za kilimo ili kuweza kupata tija.

Amesema kuwa Jeshi hilo limekuwa likifanya vizuri katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi na kijamii, ambapo amewataka kuwafikia wakulima wengi zaidi na kuwapatia elimu waliyonayo.

“Kama nyie mmeweza kulima mazao ya mbogamboga hapa na yako vizuri na hali ya hewa ya mikoa hii ni ukame, nendeni sasa mkawafuate wakulima uko uko vijijini walipo mkawapatie hii elimu na teknologia mnayotumia hapa ili waweze kuzalisha vizuri kama nyie hapa,” amesema Majaliwa.

Akiwa kwenye eneo la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Waziri Mkuu ameipongeza Wizara hiyo kwa kazi nzuri ya kupambana na Uvuvi haramu ikiwa pamoja na kuongeza Mapato ya serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here