WASHINGTON, MAREKANI
RAIS wa Marekani, Donald Trump ametangaza kuwa ataongeza ushuru wa asilimia 10 kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola bilioni 300 kwanzia Septemba 1 mwaka huu.
Tangazo hilo la Rais Trump, alilolitoa jana limejiri baada ya mazungumzo ya kibiashara kati ya Marekani na China yaliyofanyika wiki hii mjini Shanghai.
Mazungungumzo hayo yalionekana kushindwa kuzaa matunda japo Trump alisema yataendelea.
Akitangaza ushuru mpya, Rais Trump amesema China iliahidi kuongeza idadi ya bidhaa za kilimo inazonunua kutoka Marekani, lakini haijafanya hivyo.