27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli amtaka Mo Dewji kujali maslahi ya wafanyakazi wake

Anna Potinus – Dar es Salaam

Rais John Magufuli amemtaka Mfanyabishara Mohamed Dewji (Mo Dewji), kuhakikisha anajali maslahi ya wafanyakazi wake kama anayofanya katika Timu ya mpira wa miguu ya Simba Sports Club ambapo amemsihi kwamba wafanyakazi hao nao wanastahili kupata maslahi yao.

Ametoa ombi hilo leo Alhamisi Agosti 1, alipokuwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Kiwanda cha Kusaga Nafaka cha 21st Century Food and Packaging, kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam, kinachomilikiwa na mfanyabiashara huyo.

“Mohamed Dewji ninakupongeza sana katika hili na ninakuomba uwajali wananchi wanaofanya kazi hapa hasa maslahi yao kwahiyo unapokuwa unaangalia maslahi ya Simba uangalie pia masilahi ya wafanyakazi wa 21st century food and packaging,” amesema.

Aidha ameiataka Kampuni ya Metl Group iliyopo chini ya mfanyabishara huyo kuachana na utaratibu walionao wa kuagiza ngano kutoka nje ya nchi na badala yake kuanza kulima ngano nchini kwani kwa kufanya hivyo itasaudia Watanzania wanaohitaji ajira.

“Ninatoa wito kwa Kampuni ya Metl Group chini ya Mohamed Dewji, nilipokuwa ninapewa maelekezo nmeambiwa mahindi yanatoka Tanzania ambayo yanatengenezwa tani 300 kwa siku lakini ngano inayotengeneza tani 1400 kwa siku inaagizwa kutoka nje hii tuibadilishe,” amesema.

“Katika maisha yangu nilikua ninafahamu kulikuwa na mashamba makubwa sana ya ngani kule Manyara lakini sasa hivi hayatumiki na kuna wakati wawekezaji wakijaribu wanachomewa moto sasa nitoe wito hata kwa Kampuni yako muanze kulima ngano kwani mtakuwa mmesaidia Watanzania wengi,” amesema.

Aidha ametoa wito zitumike teknolojia za kawaida za uzalishaji bidhaa katika uwekezaji wa viwanda ambazo ni rahisi kwa watu kujifunza hasa katika kipindi cha mwanzo, ambapo amesema vizuri vyuo vya Veta vikawa na ushirikiano wa karibu na Shirika la kuendeleza viwanda vidogo (Sido), ili uzalishaji wa vifaa vinavyotumia teknolojia rahisi kwaajili ya viwanda vidogo vidogo vya kilimo viweze kuhusishwa hasa kwa wajasiriamali wadogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles