24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

Simba kweli neema imefunguliwa

Tima Sikilo

KLABU ya Simba imeingia mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya shilingi milioni 600 na kampuni ya Romario, ukihusisha vifaa vya mazoezi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori, alisema Dar es Salaam jana kuwa kila mwaka watakuwa wakipokea fedha taslimu shilingi milioni 100 na vifaa vya shilingi milioni 200.

“Mkataba huu, utakuwa na faida mno kwetu kwani mwaka jana tulikuwa tukitoa shilingi milioni 120 kwa kununua vifaa vya michezo, lakini msimu ujao vitatoka kwao pamoja na fedha taslim shilingi milion 100,” alisema.

Aliongeza: “Jezi tutazitangaza leo (jana) usiku saa 6:00, ambazo ndio tutazitumia msimu ujao, tutazitambulisha kupitia kurasa na mitandao yetu ya kijamii, lakini msimu huu, Romario wametutengenezea jezi aina tatu, nyekundi ambayo tutatumia nyumbani, nyeupe ugenini na kijivu ambayo itakuwa kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“jezi zetu zitaanza kuuzwa kesho (leo) katika vituo mbalimbali vya hapa Tanzania na tunaomba wapenzi na mashabiki kununua zile za halali ili siku ya Simba Day, wote tufanane pale Taifa.”

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Romario, Minhaal Dewji, alisema jezi na vifaa ambavyo watawatengenezea Simba, ni bora na imara zaidi ya vyote ambavyo wamewahi kutumia misimu iliyopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles