24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Korea Kusini kuishtaki Juventus kisa Ronaldo

SEOUL, KOREA KUSINI

MASHABIKI wenye hasira kali huko Korea Kusini wanataka walipwe fidia kutoka kwa timu ya Juventus baada ya mshambuliaji wa timu hiyo Cristiano Ronaldo kushindwa kuingia uwanjani wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Ligi K All Stars.

Nyota huyo raia wa nchini Ureno alikuwa amesaini mkataba wa kucheza dakika 45 wakati mchezo huo, lakini muda wote alionekana akiwa benchi na hakuonesha dalili za kutaka kucheza.

Kutokana na kitendo hicho cha mchezaji huyo kushindwa kuingia uwanjani, mashabiki walionekana kuchukizwa na kuanza kuimba nyimbo wakilitaja jina la hasimu wake Lionel Messi ili kumuumiza mchezaji huyo.

Mbali na hivyo, mashabiki wamekwenda mbali zaidi hadi kwenye kampuni ya sheria inayofahamika kwa jina la Myungan na kuwasilisha mashtaka yao.

Mashabiki hao wanataka walipwe ya pauni dola 59 kwa kila tiketi ya shabiki ambayo ni sawa na 135,334 za Kitanzania. Hata hivyo wakaenda mbali zaidi na kudai waongezewe milioni 1 ya fidia ya kila mmoja kutokana na kile wanachokitaja kuwa kuathirika kiakili baada ya mchezaji huyo kushindwa kuingia uwanjani.

“Kwa kawaida katika hali kama hii mlalamikaji hulipwa gharama ya tiketi, lakini swala hili ninalichukulia kama swala la kipekee kwasababu kulikuwa na matangazo ya uongo, iliwalaghai mashabiki wa nyota huyo,” alisema wakili kutoka kampuni ya mawakili katika mazungumzo na shirika la habari la Reuters.

“Kwa upande wa tatizo la kuathirika kiakili, ningependa kusema kwamba baadhi yao ni mashabiki sugu, hivyo kwao ni uchungu mkubwa kwasababu wanampenda Ronaldo.

“Kwa sasa tuna walalamikaji ambao waliishtaki kampuni, lakini nimekuwa nikipokea simu nyingi na ninadhani ni zaidi ya simu 60,000,” aliongeza.

Robin Chang, ambaye ni mkurugenzi mkuuu wa The Fasta, wakala wa Korea walioandaa mchezo huo aliangua kilio mbele ya waandishi wa habari wa kampuni ya SBS na kuthibitisha kuwa mkataba ulieleza wazi kuwa Ronaldo angecheza kwa dakika 45. Hivyo amewasaliti mashabiki 60,000 waliojitokeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles