CHRISTINA GAULUHANGA – DAR ES SALAAM
ASKARI Polisi watatu wamefariki dunia na wawili kujeuhiwa katika ajali iliyotokea kwenye Kijiji cha Kilimahewa Barabara ya Kilwa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa kipolisi Rufiji juzi na wawili kujeruhiwa.
Kati ya askari hao waliofariki dunia, mmoja anatoka Kikosi Cha Kutuliza Ghasia (FFU), wamekufa na wengine wawili wakijeruhiwa
Akizungumza na waandishi wa Habari jana jijini Dar es Salaam, Msemaji wa Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), David Misime, alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 7:30 mchana, Mkuranga.
Alisema askari hao walikuwa kwenye gari lenye namba za usajili PT.3822 aina ya Toyota Cruiser mali ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Rufiji ambapo walikuwa wakitokea Ikwiriri kwenda Kijiji Cha Mwalusembe.
Alisema wakiwamo njianigari hilo lilipasuka gurudumu la nyuma upande wa kulia na kupinduka na kusabababisha vifo vya askari vifo na majeruhi.
Waliofariki katika ajali hiyo amewataja kuwa ni Ofisa Mnadhimu wa Mkoa wa kipolisi Rufiji Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Issah Bukuku, Inspekta Esteria wa Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa kipolisi Rufiji na G.1132 Konstebo na (PC) Lameck wa Kikosi Cha Kutuliza Ghasia (FFU) Rufiji.
Misime aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na dereva wa gari hilo F.7167 Konstebo Ibrahim na F.7651 Konstebo Mgusi wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Rufiji.
Chanzo Cha ajali hiyo kimetajwa kuwa ni kupasuka kwa gurudumu la nyuma upande wa kulia na kusababisha gari kupinduka.
“Jeshi la Polisi linatoa pole kwa familia zilizopo za wapendwa wao, marafiki na wote walioguswa na tukio hilo,”alisema Misime.
Wakati huohuo, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuendelea kutii sheria na kuzingatia sheria za usalama barabarani na watakaokiuka hatua kali zitachuliwa dhidi yao.
Akizungumzia mkutano wa 39 wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), unaotarajiwa kufanyika Agosti 17 hadi 18, alisema wakuu wa nchi na Serikali kutoka nchini wanachama 16 watahudhuria ambao wataambatana na wajumbe mbalimbali.
Alisema Jeshi limejiandaa vyema kulinda raia na mali zao ili kuhakikisha mkutano huo unafanyika kwa amani tangu wageni wanaingia nchini hadi wanaondoka.