25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania wachague viongozi bora wa kupambana dhidi ya mimba za utotoni

Na Brighiter Masaki

Wakati Taifa linajiandaa kwenda katika Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za mitaa, wananchi wametakiwa kuchagua viongozi watakaopinga mimba za utotoni.

Wito huwo umetolewa kwa wananchi kuhakikisha wanatumia haki yao ya msingi kwa kupiga kura za kuchagua Viongozi wenye hofu ya Mungu na wanaojali haki za Watoto wa Kike.

Akizungumza mapema Leo, Mratibu wa Shirika la utetezi wa haki za mtoto wa kike la New Hope Tanzania Elizabeth Ngaiza, amesema kuwa katika Kampeni ya ‘Niache Nisome Kwanza’ itawasaidia watoto wakike kusoma kwa bidii.

“Niache nisome kwanza ni kampeni ya kusaidia watoto wa kike na kupinga mimba za utotoni, nimebaini uwepo wa baadhi ya viongozi wa Ngazi za mitaa wasiokuwa na weledi, wasiowajibika na hawawezi kusimama katika nafasi yao ya kutetea haki za mtoto wa kike”anasema Elizabeth .

Aidha Elizabeth Ngaiza amesema lengo la Kampeni ya “Niache Nisome Kwanza” ni kupambana na mimba za utotoni kwa mtoto wa kike na kuhakikisha anawekewa mazingira wezeshi ya kusoma pasipo changamoto wala vikwazo vyovyote.

Hata hivyo Ngaiza amewaomba wadau na wananchi kuendelea kumuunga mkono katika Kampeni ya Kumlinda mtoto wa kike apate elimu Bora kwakuwa anaamini ukimwezesha mwanamke kupata elimu itasaidia kuinua kipato cha Familia na Taifa kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles