28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli awaonya watumishi wanaoenda kutibiwa nje

Anna Potinus

Rais John Magufuli amemtaka Waziri wa Afya Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuanza kudhibiti matumizi ya watumishi waokwenda nje ya nchi kwaajili ya matibabu kwakua wengi wao hutumia fursa hiyo ili kujipatia safari na kwenda kutalii.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Julai 15, wakati akizungumza na wananchi katika hafla ya uzinduzi wa miradi saba ya maendeleo ya huduma za tiba katika hospitali ya rufaa ya Bugando Mkoani Mwanza ambapo amesema kuwa hakuna sababu ya kwenda nje wakati magonjwa hayo yanatibika hapa nchini.

“Kupeleka wagonjwa nje kwa Watanzania ilikua ni dili hasa kwa watendaji, wapo waliokuwa wanapewa vibali kwenda kutibiwa India lakini anaumwa mafua kusudi tu apate safari na apate msindikizaji na akifika kule anaandika dawa ambazo hata hanywi halafu bili zote zinaletwa zije kulipwa na serikali,” amesema.

“Waziri wa Afya nenda kafuatilie malipo yote tunayotakiwa kulipa kule India na ukikuta malipo ya mtu ambae hakuwa mgonjwa akazilipe mwenyewe ni lazima tujenge nidhamu katika nchi yetu, hatukatai mtu kupelekwa nje lakini apelekwe kwa magonjwa ambayo yameshindikana hapa,” amesema.

“Wapo wagonjwa wanaoomba kwenda nje halafu wanaenda kuripoti hospitalini kasha wanaenda kukaa hotelini wakiwa wamesindikizwa na wake zao, rafiki zao au waume zao sasa ni lazima tuanze kudhibiti matumizi ya watu wanaokwenda nje kutibiwa hakuna sababu ya kwenda nje wakati magonjwa hayo yanatibika hapa,” amesema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles