25.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

IGP atangaza kiama kwa askari wapenda rushwa

NA SHOMARI BINDA-MUSOMA

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amewataka askari wote kuzingatia nidhamu na kujiepusha na vitendo vya rushwa katika utendaji wao wa kazi na kwamba watakaoshindwa kufuata misingi hiyo, hawatakuwa na nafasi.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini Musoma, wakati akifanya ukaguzi wa majengo mapya ya ghorofa ya nyumba za askari.

IGP Sirro alisema wapo askari ambao bado hawataki kuzingatia taratibu za kinidhamu zinazotakiwa na kamwe hawezi kuwavumilia kama hawataweza kubadilika.

Alisema nidhamu ndiyo jambo la msingi kwa askari popote alipo na anapokuwa akitekeleza majukumu yake ya kila siku.

IGP Sirro alisema licha ya nidhamu lipo suala la rushwa ambalo pia limekuwa likimchukiza na kuwataka askari kujiepusha na masuala ya kuomba na kupokea rushwa.

Alisema bado wapo askari ambao hawataki kubadilika na kuachana na vitendo vya rushwa na kudai kamwe hawatakuwa na nafasi ya kulitumikia jeshi hilo.

“Kila askari lazima ajitambue na kutimiza wajibu wake, usisubiri kusukumwa kama ambavyo mimi sisubiri kusukumwa, tufanye kazi kwa weledi mkubwa popote pale tulipo.

“Wapo askari ambao hawajitumi katika utendaji kazi, wao, pia wabadilike warudi kwenye mstari na naamini baada ya hapa mambo yatakaa vizuri,” alisema IGP Sirro.

Aidha alisema katika suala la utayari, askari wapo vizuri na kuwapongeza kwenye eneo hilo na kuishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa ujenzi wa nyumba za askari kote nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles