Kamishna Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Dk. Alan Kijazi, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Wahariri na Wanahabari Waandamizi jijini Mwanza.
Na Eliya Mbonea, Mwanza
Kamishna Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Dk.Allan Kijazi amesema watalazimika kutumia ubabe kwa wote wanaotaka kuvuruga utalii nchini.
Kauli hiyo ameitoa leo Julai 4, jijini Mwanza kwenye mkutano wa mwaka wa TANAPA, Wahariri na Wanahabari Waandamizi uliofunguliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kigwangala.
Akiwasilisha Mada ya Chimbuko na maana ya kuanzishwa mfumo wa Jeshi Usu linalosimamia uhifadhi na misitu Dk.Kijazi amesema tayari wameanza kuona mafanikio ya kuanzishwa kwa mfumo huo.
“Maeneo mengi ujangili umedhibitiwa tunakwenda vizuri mpaka sasa, wanaotaka kuvuruga utalii wetu tutawatisha kwa vifaa vyetu,” amesema Dk.Kijazi.