Christina Gauluhanga, Dar es Salaam
Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido), limefanikiwa kuongeza idadi ya wawekezaji , ubunifu na ajira kupitia mfumo wa Kongano.
Akizungumza leo Julai 4, katika Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba (DITF-), Mkurugenzi Maendeleo ya Teknolojia na Uendelezaji Viwanda, Mhandisi Emmanuel Saiguran amesema, Kongano hilo lilianza Mwaka 2006.
Amesema Sido limelenga kuwasaidia wajasiriamali wa ndani ili waweze kufikia malengo yao.
Saiguran amesema Shirika la Maendeleo la watu wa Japan (Jica), wanasimamia Kongano tano na Shirika la Maendeleo la Marekani (Sida), wanasimamia Kongano 15 ambapo mbili zipo Visiwani Zanzibar na 13 Tanzania Barabarani.