32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri atatua mgogoro wa wachimbaji wadogo, mwekezaji

Issa Mtuwa -Dodoma

WAZIRI wa Madini, Doto Biteko, amesema Serikali itahakikisha inasimamia haki kwa wawekezaji wote bila kujali kama ni raia wa kigeni ama kutoka nje.

Alitoa kauli hiyo jana jijini hapa, wakati akisuluhisha mgogoro baina ya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu eneo la Ikungi mkoani Mara na mwekezaji Kampuni ya PolyGold (T) Ltd.

Jana baada ya Biteko kusikiliza pande zote mbili na kubaini tatizo lilikuwa kwa wachimbaji wadogo alisema; “Niwaambie ukweli, huyu mnaemuona (mwekezaji) ana haki kama nyinyi, akionewa huyo mjue ana watu nyuma yake.

“Ana ubalozi hapa, kwa hiyo siko teyari kuchafua jina la Serikali na wizara ninayoiongoza kwa kukiuka haki ya upande fulani.

“Uwe mzawa, uwe mwekezaji wa nje, kwangu haki yako utaipata, kwa hiyo kaeni na mkubaliane na mwekezaji wenu, mimi na wenzangu tunatoka tunawacha, nikirudi tupate majibu, msimamo wangu nimewapa,” alisema Biteko.

Mara baada ya maelekezo hayo, wachimbaji wadogo wakiongozwa na Edwin Mchihiyo na Sosy Mgonya ambaye leseni yake imenusurika kufutwa na waziri, walikaa pamoja na Kampuni ya PolyGold (T) Ltd iliyowakilishwa na Sergey Sagsyan na Benny Haule na kuzungumza kuhusu mvutano juu ya mgogoro wao na kufikia mwafaka.

Akiongea kwa niaba ya wenzake, Mchihiyo alimshukuru Waziri Biteko kwa kusimamia kutatua mgogoro wao ambao umefikia tamati na kuahidi wanakwenda kutekeleza makubaliano yaliyokuwa yanaleta sintofahau baina yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles