29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Juma Nature: Nitagombea ubunge 2020

maxresdefaultNA FESTO POLEA

KIONGOZI wa kundi la Wanaume Halisi, Juma Kassim Nature, amesema matarajio yake ya kugombea ubunge yatatimia mwaka 2020 atakapogombea rasmi katika jimbo mojawapo nchini.

Nature aliwahi kutangaza nia ya kugombea ubunge kwa mwaka huu lakini hakutekeleza hilo badala yake akawa mpiga kampeni wa wasanii wenzake na viongozi mbalimbali waliokuwa wakigombea nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Mwaka huu nilikuwa najifunza mambo mengi kupitia viongozi waliokuwa wakigombea nafasi mbalimbali na nimeshajifunza na naendelea kujifunza ila ikifika 2020 nami nitagombea ubunge’’ alisema Nature.

Akizungumzia kazi zake mpya, Nature alisema zitaanza kusikika hivi karibuni kwa kuwa alikuwa akisubiri uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani uishe.

“Kuanzia mwezi huu mashabiki wangu watarajie nyimbo mpya kwa kuwa nilikuwa nasubiri uchaguzi uishe ndiyo nitoe nyimbo mpya na umeshaisha sasa nitatoa siku za karibuni,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles