MKE wa msanii wa hip hop nchini Marekani, Kanye West, Kim Kardashian, ameweka wazi kwamba anashindwa kula kwa mpangilio kwa kuwa huwa anahisi njaa mara kwa mara.
Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 35, anatarajia kupata mtoto wa pili, awali mrembo huyo alikuwa akifuata ratiba ya mlo kamili lakini kwa sasa imeshindikana.
“Kwa hatua niliyofikia kwa sasa nahisi mtoto nitakayejifungua atakuwa anakula sana kama ninavyokula mimi mara kwa mara bila kuwa na mpangilio wa chakula,” alieleza Kim Kardashian.
Alifafanua ratiba yake kwamba alikuwa akila yai, parachichi na kipande cha mkate kila alipoamka lakini kwa sasa njaa imemuharibia ratiba hiyo kwa kuwa anakula zaidi ya hivyo,” alisema Kim.