SAMWEL MWANGA-MASWA
Baadhi ya wazazi Wilayani Maswa, Mkoani Simiyu wameshauri serikali kuwa na utaratibu wa kuwapima ujauzito wanafunzi wa kike kuanzia darasa la nne hadi kidato cha sita mara kwa mara kutokana na kasi ya wanafunzi wa kike katika shule za msingi na sekondari kupatiwa ujauzito.
Wakizungumza na MTANZANIA leo Juni 18, wazazi hao wamesema kuwa ili kuunga mkono jitihada za Mkuu wa wilaya ya Maswa Dk
Seif Shekalaghe za kupambana na mimba za utotoni kwa wanafunzi
wilayani humo njia pekee ya kukabiliana na tatizo hilo ni kuanza utaratibu wa kuwapima ujauzito wanafunzi hao wanapokuwa mashuleni.
“Vita hii ya kupambana na mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari si ya Mkuu wa wilaya pekee hivyo inapaswa kuungwa mkono na watu wote kuanzia ngazi ya familia ili kuhakikisha kuwa tatizo hilo linamalizika katika wilaya yetu ya Maswa,”
“Katika wilaya yetu tuna tatizo kubwa la wanafunzi wa kike hasa wa shule za msingi kutomaliza masomo yao kwa kupatiwa ujauzito, suala hili linachangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa kiwango cha elimu sasa ufike wakati wa kulikomesha,” anesema mmoja wa wazazi, Zawadi Kaijage.
Aidhya walisema kuwa ili kufanikisha suala hilo ni vizuri idara ya idara ya elimu ikishirikiana na idara ya afya wilayani humo ikaamua kufikia hatua hiyo yenye lengo la kudhibiti vitendo vya ngono kwa wanafunzi walioko katika madarasa hayo kwakua wengi wao wana umri wa kati ya miaka minane hadi 16.