RAPA wa kundi la Maybach Music, Rick Rose na kiongozi wa kundi la G Unit, 50 Cent, bifu lao limefikia pabaya baada ya Rick Rose kueleza kwamba 50 Cent amefilisika kimuziki.
50 Cent aliwahi kusema kwamba amefilisika ili asaidiwe ama kufilisiwa mali zake kutokana na madeni anayodaiwa, ndipo Rick Rose alipotumia maneno yake kumshambulia huku akisema kuwa 50 Cent hana kitu na ameanza kufanya biashara ya nguo badala ya kufanya muziki.
Bifu hili limeendelea zaidi huku 50 Cent akidai anao mkanda wa ngono unaomuonyesha mpenzi wa Rick Rose akifanyiwa kitendo hicho.
Hata hivyo wawili hao wameanza kutambiana kwa kushindanisha mali wanazomiliki, huku 50 akidai kwamba mbali na muziki ana biashara mbalimbali ambazo zinamuingizia fedha nyingi kwa mwaka dhidi ya Rick Ross.