26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wanafunzi wa kike 1,119 wapata ufadhili Tabora

Na ALLAN VICENT

-TABORA

JUMLA ya wanafunzi wa kike 1,119 wa shule za sekondari wanaotoka katika familia zisizo na uwezo mkoani hapa wamepata ufadhili wa kielimu kutoka Shirika la CAMFED lenye makao yake makuu Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ofisa Elimu Taaluma, Aron Vedasto, alisema wanafunzi hao wanatoka katika shule mbalimbali zilizopo katika wilaya za Tabora Manispaa na Nzega. 

Alisema katika ufadhili huo,  shirika linawapatia mahitaji yote ya shule ikiwemo sare za shule, viatu, madaftari, taulo za kike, usafiri kwa wale wanaotoka mbali, godoro, blanketi, neti na fedha ya matumizi kwa wale wa bweni.

Alibainisha kuwa wanafunzi wanaofadhiliwa na mradi huo wanatoka katika shule za sekondari 19 zilizoko katika wilaya hizo mbili ambapo shule 11 ni za Halmashauri ya Manispaa ya Tabora na nane za Halmashauri ya Wilaya ya Nzega.    

Vedasto aliongeza kuwa shirika hilo limekuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi hao na halmashauri zao kwani kwa mwaka huu tu zaidi ya shilingi milioni 252 zimetolewa kwa mahitaji yao na kuboreshwa miradi ya shule zao.  

‘Ufadhili wa CAMFED kwa wanafunzi hawa umekuja wakati mwafaka, kwani maono ya mkuu wetu wa mkoa ni kuhakikisha kila familia hapa Tabora inakuwa na msomi wa chuo kikuu, hivyo ufadhili huo ni wa kujivunia sana,” alisema.

Ofisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Tabora, Chatta Luleka, alisema shirika hilo limekuwa msaada mkubwa kwa watoto hao kwani kila mmoja anapewa kiasi cha Sh 250,000 kwa mahitaji yake na hilo limewapa hamasa na bidii ya kusoma.

Mwalimu mlezi wa wanafunzi wanaonufaika na mradi huo kutoka Shule ya Sekondari Skanda, Zabibu Gregory, alisema CAMFED ni shirika lisilo la kiserikali linalosaidia watoto wa kike walio katika mazingira magumu.

Alisema msaada na elimu inayotolewa na shirika hilo vimekuwa chachu kubwa kwa wanafunzi hao kujitambua, kubadili tabia zao, kusoma kwa bidii na kuelimisha wenzao watumie vizuri elimu wanayopata.

Baadhi ya wanufaika wa ufadhili huo, Mwanne Daudi Said (Isevya Sekondari) na Therezia Hamis (Sikanda Sekondari) walisema msaada huo umekuwa mkombozi kwao na elimu wanayopewa na shirika hilo imewapa ujasiri mkubwa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles