33.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 28, 2024

Contact us: [email protected]

Simba, KMC zamuweka njia panda Rashid

Na MOHAMED KASSARA

-DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI  wa Simba, Mohamed Rashid  amesema kwa sasa yuko njia panda, baada ya mkataba wake kucheza kwa mkopo KMC kufikia tamati.

Tangu alipojiunga na Simba kwa mkataba wa miaka mitatu msimu uliopita akitokea Tanzania Prisons,Rashid amekosa namba ya kudumu katika kikosi cha Wekundu hao, hatua iliyoifanya klabu hiyo imtoe kwa mkopo KMC ambako ameisaidia kumaliza msimu katika nafasi ya nne.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Rashid  alisema hatua ya KMC kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao,  kinamfanya kutamani kuendelea  kuichezea timu hiyo, lakini anajikuta katika wakati mgumu kutokana na kutakiwa pia na mwajiri wake, Simba.

“Ni kweli nipo katika wakati mgumu wa kufanya maamuzi, nilikuwa na bahati nzuri sana  katika kipindi changu cha kuitumikia KMC kwa mkopo, nilipata nafasi ya kucheza mara kwa mara, hiki ni kitu ambacho  kila mchezaji anakihitaji, bahati nzuri tulipambana na kuisadia timu kumaliza nafasi ya nne, na sasa imepata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa, natamani kuipata fursa hiyo.

“Viongozi wa Simba wamenipigia wakinihitaji nirudi, sina tatizo sana kurejea, hofu yangu ni juu ya nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza, hapo ndipo ninapopata mashaka, bado naendelea kuongea nao ili kuona kama wataridhia nibaki KMC,”alisema Rashid 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles