27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha Prisons aiparura Bodi ya Ligi

NA MOHAMED KASSARA

-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Tanzania Prisons, Adolf Rishard ameitaka Bodi ya Ligi (TPBL), iwe makini wakati wa kupanga ratiba ya Ligi Kuu msimu ujao,  ili kuepusha mrundikano wa viporo na malalamiko  kama ilivyokuwamsimu uliopita.

Rishard aliinusuru Prisons kushuka daraja msimu uliopita, baada ya kurithi mikoba ya mtangulizi wake, Mohamed Abdallah ‘Bares’ aliyetimuliwa kutokana na mwenendo mbaya uliosababisha timu hiyo kuwa katika tishio la kushuka daraja.

Rishard aliichukua timu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Magereza Tanzania, ikiwa katika nafasi ya 19 miongoni mwa timu 20, katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Lakini hadi inamaliza msimu, Prisons ilikuwa katika nafasi ya 12, baada ya kuvuna pointi 46.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Rishard alisema kama  bodi ya ligi inataka kuondoa mambo yaliyochafua taswira ya Ligi Kuu msimu uliopita, inapaswa kuiangalia kwa makini ratiba.

 “Msimu uliopita ulikuwa na changamoto nyingi, nyingine zilitokana na ongezeko la timu, hata hivyo suala la ratiba lilikuwa kikwazo kikubwa, ratiba ilikuwaya  hovyo, haikupangwa vizuri, haikuzingatia hali ya kiuchumi ya timu, pia ilikuwa ikivurugwa mara kwa mara, jambo lililosababisha viporo vingi kwa baadhi ya timu.

“Bodi la Ligi iliangalie suala hili kwa upana wake, haiwezekani timu inacheza Dar es Salaam alafu baada ya siku moja tena icheze Mbeya, hiyo ilitutokea, tulipotoka kucheza na Yanga Uwanja wa  Uhuru kisha tukacheza na Simba, Sokoine baada ya siku mbili.

Ratiba ipangwe kama zamani, timu inacheza mechi zake kwa kanda, wahusika  warekebishe  mapungufu yaliyojitokeza ili yasijirudie msimu ujao,”alisema kiungo huyo wa zamani wa Taifa Stars.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles