30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

UWAJIBIKAJI, NIDHAMU ZAFYEKA MKUDE, AJIB STARS

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Emmanuel Amunike amewatema katika kikosi chake hicho kinachojiandaa na fainali za mataifa ya Afrika, wachezaji saba wakiwemo Jonas Mkude na Ibrahim Ajib.

Kikosi cha Stars kiliondoka nchini jana kikiwa na wachezaji 32, kwenda Misri ambako kitashiriki fainali za Afcon zitakazoanza kutimua vumbi  kuanzia Juni 21 hadi 19 mwaka huu nchini humo.

Wachezaji wengine waliotemwa katika katika hicho ni Kenned Juma, Ayoub Lyanga, Ally Khamis, Ally Ally na Shomary Kapombe ambaye ni majeruhi.

Akizungumza jana baada ya kumalizika kwa mazoezi ya mwisho yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Amunike alisema anafahamu wanaenda kucheza michuano mikubwa lakini wanaamini watafanya vizuri na kuleta matokeo yenye utofauti .

“Tulianza mazoezi Jumapili, nimeweza kuwaangalia wachezaji wote ambao waliweza kujituma na kuonyesha kiwango kizuri kwenye mazoezi ikiwemo pia na nidhamu.

“Sijachagua mchezaji kwa kuangalia ukubwa wa jina au kwa sababu anapendwa na mashabiki , nimeangalia ana mchango gani kwenye timu na ataisaidia vipi kwani tunakabiliwa na michuano mikubwa.

“Tunatakiwa kuangalia kwa ukubwa, hii ni timu ya Taifa  na bila nidhamu huwezi ukafanikiwa kwenye mpira hivyo anaamini kikosi nilichokichagua kitaleta matokeo yenye utofauti na kufanya vema,”alisema Amunike.

Amunike alisema, anafahamu mchezo wa kwanza wataanza dhidi ya Senegal, timu  inayoundwa na wachezaji wakubwa akiwemo Sadio Mane anayekipiga katika klabu ya Liverpool ya England, lakini hilo haliwatishi kwakua wao pia wamejiandaa kiasi cha kutosha.

“Hata sisi tuna wachezaji wazuri kama Mbwana Samatta, Simon Msuva, Faridi Mussa na wengine ambao hawana majina makubwa lakini wana uwezo mkubwa, matokeo yataonekana uwanjani.

“Nafahamu michuano hii ina presha kubwa lakini tutatumia  kambi yetu ya wiki mbili kujiweka fiti, tutacheza mechi mbili za kirafiki ikiwemo dhidi ya Misri pamoja na Zimbabwe,”alisema kocha huyo ambaye ni  staa wa zamani wa Bareleno na timu ya Taifa ya Nigeria(Super Eagle).

Taifa Stars ilifanikiwa kufuzu michuano hiyo, baada ya kuifunga Uganda mabao 3-0, katika mchezo mwisho wa michezo ya kufuzu uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Katika fainali hizo, Taifa Stars imepangwa kundi C, pamoja na Algeria, Senegal na majirani zao Kenya (Harambee Stars).

Itafungua dimba dhidi ya Senegal maarufu kama Simba wa Teranga Juni 23, kabla ya kuivaa Kenya katika mchezo utakaofuata.

Hiyo itakuwa mara ya pili kwa Stars kuchiriki Afcon, mara ya kwanza ilikuwa katika fainali zilizofanyika mwaka 1980 nchini Nigeria

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles