25.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

DC ampa miezi miwili mkandarasi kukamilisha ujenzi wa kituo

Na Derick Milton, Bariadi

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Festo Kiswaga ametoa muda wa miezi miwili kwa mkandarasi anayejenga stendi mpya ya mkoa kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo ndani ya muda huo.

Ujenzi wa stendi hiyo umegharimu Sh bilioni 7.2 na unatekelezwa na mkandarasi Kings Builders na Construction Co. Ltd kutoka Dar es salaam ambapo umefikia asilimia 68 ya ujenzi wake.

Kiswaga ametoa agizo hilo leo Ijumaa Juni 7, baada ya kutembelea mradi huo, ambapo alisikitishwa kuona ujenzi umesimama kwa muda wa mwezi mmoja bila ya sababu za msingi.

“Mradi huu ulitakiwa kukamilika Mei, mwaka huu lakini hadi leo bado ujenzi haujakamilika, fedha zipo, mkandarasi umelipwa zaidi ya Sh bilioni tatu, lakini kazi zimesimama, ndani ya miezi miwili nataka ujenzi ukamilike,” amesema Kiswaga.

Kiswaga pia amemuonya miandarasi huyo endapo hatakamilisha ujenzi huu ndani ya muda huo hatua kali zitachukuliwa ikiwamo kuvunjwa kwa mkataba kwani sababu zilizotolewa hazina msingi wananchi na serikali tunachotaka ni mradi ukamilike.

Kwa upande wake mwakilishi wa mkandarasi, Mhandisi Charles Lyamuya, aliahidi kutekeleza maagizo ya Mkuu wa Wilaya huku akieleza sababu za kusimama kuwa ni kuchelewa kwa kibali cha kutozwa Kodi Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye vifaa vya ujenzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles