25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Wadau watakiwa kutumia Bandari ya Mwanza kuepuka gharama

Esther Mbussi, Mwanza

Wafanyabiashara, wadau wa bandari na wasafirishaji wa shehena za mizigo kutoka nchi mbalimbali, wameshauriwa kutumia Bandari ya Mwanza kutokana na bandari hiyo kuwa ya gharama nafuu na kutumia muda mfupi kuliko zote.

Kaimu Meneja wa Bandari ya Ziwa Victoria, Geofrey Lwesya, amesema hatua hiyo ni kwa sababu Bandari ya
Mwanza Kusini ndiyo inawaunganisha na Bandari zote za Ziwa Victoria.

“Tuna gati za kisasa, vitendea kazi vya kutosha na sisi ndiyo wenye bei nafuu kuliko wote na tunatumia muda mfupi.

“WFP ni mteja wetu mkubwa ambapo wanatumia Bandari ya Isaka kusafirisha chakula mara kwa mara kwenda Sudan Kusini, lakini pia Rwanda, Burundi na Uganda nao ni wadau wetu wakubwa,” amesema.

Lwesya pia amesema kumekuwapo na mikakati mbalimbali ili kuendana na mahitaji ya wateja na soko lililopo ikiwamo kuendelea na wateja waliopo, kutafuta wateja wapya na kurudisha walioondoka kwenye soko na kuzidisha wateja wakubwa.

Ametaja mikakati mingine ni kurasimisha bandari binafsi, ununuzi wa vifaa vipya kwa ajili ya ubebaji wa mizigo na kuajiri wafanyakazi wapya ili kuimarisha utendaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles