22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Trump: Uingereza ikiachana na EU itapata dili zuri Marekani

LONDON

-Uingereza

RAIS wa Marekani, Donald Trump amesema anaamini  Uingereza baada ya kuachana na Umoja wa Ulaya (EU)inaweza kuwa na dili zuri sana la biashara na Marekani.

Trump ambaye jana alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kiserikali nchini Uingereza aliyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa wafanyabiashara katika mkutano ulioandaliwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Theresa May.

Katika mkutano wao wa pamoja walioufanya na waandishi wa habari baadae jana, Trump pia alieleza kuwa Marekani na Uingereza zimekuwa na ushirikiano ambao haujapata kutokea.

May naye alisema walikuwa na uhusiano mkubwa ambao wanapaswa kuujenga.

Trump na May pia walikuwa na mazungumzo  muhimu likiwamo suala la agenda ya kibiashara na Huawei.

Wakati Marekani ina mgogoro na kampuni ya teknolojia ya China ya Huawei,  Uingereza inaelezwa inaweza kuruhusu kusambaza vifaa vyake vya kwa ajili ya 5G.

Katika mkutano na wafanyabiashara uliowakutanisha pia kampuni tano kubwa za Uingereza na Marekani, mawaziri na maofisa waandamizi May alisisitiza kuwa kulikuwa na fursa kubwa kwa Uingereza na Marekani kufanya kazi pamoja kwa ajili ya siku za baadae.

Wakati huo huo jana waandamanaji walikusanyika katikati ya London huku sauti za kupinga ziara yake zikisikika.

Maandamano kama hayo pia yalipangwa kufanywa Birmingham, Stoke, Sheffield, Glasgow, Edinburgh, Chester, Leicester, Oxford na Exeter.

Polisi nchini Uingereza imesema zaidi ya maofisa 3,000 wamesambazwa kwa ajili ya ziara hiyo ya Trump inayomalizika leo.

Kiongozi wa chama cha Labour Jeremy Bernard Corbyn ambaye alisusia hafla ya chakula cha jioni na Trump  naye aliungana na waandamanaji na vyama vingine vya siasa ikiwamo Liberal Democrats na  Green Party.

Alisema hakukataa kuonana na Trump isipokuta alikuwa akitaka mazungumzo.

Corbyn alimkosoa Trump kwa kumshambulia Meya wa London Sadiq Khan. 

“Najivunia jiji letu lina Meya ambaye ni Muislamu, kitu ambacho tunaweza kukiondoa ni Islamophobia, na aina nyingine yeyote ya ubaguzi.

Juzi mara baada ya kutua katika ardhi ya London, Trump alirusha kombora kupitia akaunti yake ya Twitter  dhidi ya Meya  huyo wa London, Sadiq Khan akisema ni ‘Jiwe potevu la baridi’.  

Ujumbe huo wa rais Trump kwa Khan ambao ulisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, ulieleza kuwa Khan;  “amefanya kazi mbaya na ya kijinga  kama Meya wa London na kwamba anatakiwa kujielekeza kupambana na uhalifu na si  kushambulia yeye Trump’. 

Khan amekuwa akimshutumu Trump kama ni fashisti wa karne ya 21 ambaye hapaswi kukaribishwa Uingereza.

“Khan ananikumbusha sana kuhusu meya wetu asiye na uwezo wa Jiji la New York, de Blasio (Billy de Blasio),  ambaye naye amefanya kazi mbaya –nusu tu ya urefu wake (Khan). Kwa namna yeyote natarajia kuwa rafiki mzuri wa Uingereza, natua sasa’, alindika Trump wakati anawasili Uingereza.  

Kauli hiyo ya Trump dhidi ya Khan ilibiwa na msemaji wa Meya huyo wa London aliyesema “matusi ya kitoto ” yanapaswa kuwekwa kando na Rais wa Marekani,”.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles