25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Ulega ‘atangaza’ dawa ya kitambi bungeni

Ramadhan Hassan, Dodoma

Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega, amesema njia bora ya kupambana na kitambi ni kujikinga kutokukipata kwa kuhakikisha unazingatia ulaji vyakula unaofaa na ufanyaji mazoezi.

Ulega amesema hayo bungeni leo Mei 29, kwa niaba ya Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Khadija Ali (CCM) lililoulizwa na Mbunge wa Mlalo Rashid  Shangazi (CCM).

Katika swali lake Shangazi alitaka kujua kama uzito mkubwa wa mwili ni dalili za mwanzo za magonjwa yasiyo ya kuambukiza, je serikali ina makakati gani wa kupambana na magonjwa hayo na mbali na mzoezi ni mbinu gani nyingine za kitaalamu za kupambana na kitambi?

Akijibu swali hilo Ulega amesema Wizara ya Afya mwaka 2011 ilianzisha rasmi kitengo cha kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa lengo maalumu la kukinga na kudhibiti magonjwa hayo.

“Tumetengeneza mpango mkakati 2016/20 wa kupambana na magonjwa hayo ambao umeweka bayana malengo, mikakati na utekelezaj.

“Utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu magonjwa haya kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo vipeperushi, redio, runinga, mitandao ya kijamii na nyinginezo ili kuongeza uelewa kwa jamii,” amesema Ulega.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles