27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Iran: Hatuoni uwezekano wa kuzungumza na Marekani

TEHRAN, IRAN

SERIKALI ya Iran imesema haioni uwezekano wa kufanya mazungumzo na Marekani.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Mousavi alisema hayo jana, siku moja baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kusema upo uwezekano wa kufikia makubaliano na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Hata hivyo, Mousavi alinukuliwa na Shirika la Habari la Iran, Fars akisema Iran haitilii maanani maneno hayo bali kile ambacho ni muhimu kwa Iran na mabadiliko ya namna suala hilo linavyoshughulikiwa.

Awali Trump alisema anaamini Iran itapenda kuwa na makubaliano na anafikiri hilo ni wazo zuri na kuna uwezekano wa hilo kufanyika.

Mzozo umezidi kuongezeka kati ya Marekani na Iran tangu Marekani ilipozipeleka ndege zake za kivita na silaha nyingine Mashariki ya Kati.

Aidha Trump alitangaza mipango ya kuwapeleka wanajeshi 1,500 zaidi katika eneo hilo, hali ambayo imeibua hofu ya vita.

Marekani ilijiondoa katika mkataba wa kimataifa kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, na ikaongeza vikwazo dhidi ya Iran.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles