- Ni baada ya mvua kuharibu miundombinu
ANDREW MSECHU-DAR ES SALAAM
JIJI la Dar es Salaam, linakabiliwa na changamoto ya miundombinu, hali inayoifanya kila mara Serikali kuweka mikakati ili kuweza kupanga upya miundombinu yake.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuharibika kwa miundombuni hasa ya barabara kutokana na mvua zinazoelendea kunyesha, huku jiji hilo kwa sasa likikadiriwa kuwa na idadi kubwa ya wakazi wake wanaokisiwa kufika zaidi ya milioni tano.
Kutokana na athari hizo za mvua za masika zinazosababisha kuharibika kwa miundombinu, MTANZANIA imezungumza na Mratibu wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijiji Mkoa wa Dar es Salaam (Tarura), Mhandisi George Tarimo, ambapo alisema tatizo linalosababisha uharibifu wa barabara ni kutokuwa na mipango miji inayoheshimu njia za asili za maji, hivyo maji kukwama katika baadhi ya maeneo na kulazimisha njia.
Alisema maeneo mengi ambayo yanaathiriwa na mafuriko na mkwamo wa maji ya mvua yanatokana na watu kujenga kiholela, hata katika maeneo ambayo awali yalikuwa na mpangilio mzuri, jambo lililosababisha uharibifu wa miundombonu ya barabara.
Mhandisi Tarimo alisema katika hilo ni vyema wananchi wawe wa kwanza kuhakikisha wanaacha kutumia uwezo wao walio nao kujenga nyumba kwenye mikondo ya maji na kuzuia njia za maji, kwa kuwa hasara inayotokana na hatua hizo ni kubwa na inayojirudia kila mara.
Alisema kwa sasa wanaendelea kufanya tathmini ya athari zinazosababishwa na mvua katika maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam, ambapo kwa sasa wameshakamilisha katika baaadhi ya maeneo.
“Tunaendelea kufuatilia athari zinazohitaji dharura na zile zinazohitaji uharaka. Tuko tayari kuchukua hatua za dharura kama kuna sehemu labda daraja limezolewa na maji na kukatisha mawasiliano, ambapo hatua zake ni kutengeneza kivuko cha dharura lakini kuangalia uwezekano wa kupata daraja jipya kwa haraka,” alisema.
Alisema tayari wameshafanya tathmini ya awali katika barabara zote zinazosimamiwa na Tarura na kupeleka taarifa makao makuu kwa ajili ya kufanyiwa upembuzi na kupatiwa fedha.
Alisema mtandao wa barabara za Tarura Jijini Dar es Salaam una urefu wa Kilometa 4,234.098 ambapo kati ya hizo, Kilometa 320.586 ni za lami, kilometa 1,149.368 ni za changarawe na Kilometa 2,763.853 ni za udongo.
Kuhusu matengenezo
Alisema kwa sasa, kwenye barabara za lami tayari wakandarasi wameshapewa agizo la utayari na wameshaanza kuchukua hatua za awali za dharura kwa kuzuia mashimo kwa kuweka vifusi ili kuruhusu magari kuendelea kutumia barabara hizo.
Alisema barabara nyingi za lami zimepata mashimo kwa hiyo mvua zitakaposimama tu kazi ya kuziba mashimo hayo zitaanza, kwa kuwa kazi hiyo haiwezi kufanyika wakati mvua zikiendelea kunyesha.
“Kwa hizi barabara za lami, fedha tayari ipo na wakandarasi wameshaambiwa wajiandae, mvua ikitumia tu kwa siku mbili au tatu watu wataanza kuona kazi ikifanyika. Ila kwa barabara za changarawe bado zinahitaji kusubiri mvua iishe na maji yakauke,” alisema.
Gharama
Alisema kutokana na uharibifu huo, tathmini ya awali inaonyesha kuwa zinahitajika Sh bilioni 9.2 kwa ajili ya kukarabati barabara za changarawe na za vumbi katika maeneo yote, lakini gharama hiyo inaweza kuongezeka katika tathmini inayoendelea.
Alisema katika barabara za lami ambazo zinahitaji kuzibwa mashimo, tathmini ya awali inaonesha kuwa gahrama yake inafikia Sh milioni 892.2 ambazo tayari Tarura Makao Makuu wameshawahakikishia kuwapa fedha hizo kwa ajili ya ukarabati.
Alisema kuna baadhi ya barabara za changarawe ambazo tayari mpango wa kuziboresha ka kiwango cha lami na za vumbi ambazo zilishaingizwa kwenye mpango wa kuziboresha kwa kiwango cha changarawe ulishaingizwa kwenye bajeti ya mwaka huu ikiwemo barabara ya Pugu Majohe, Makonde na ya Kitunda Kivule-Msongola.
Tanroads watoa neno
Akizungumzia athari zinazotokana na mvua zinazoedelea jijini Dar es Salaam, Msimamisi wa Matengenezo ya Barabara Tanroads Dar es Salaam, Mhandisi Eliamin Tenga alisema hadi sasa hakuna barabara iliyokuwa chini yao ambayo imekatika.
Alisema athari zinazoonekana ni za barabara kupata mashimo kwa viwango tofauti na kwamba barabara kuu zimeathirika kwa kwa kiasi kidogo na tayari zimeshazibwa kwa asilimia 90 na kwa barabara za mkoa ndizo zilizoathirika kwa kiwango kikubwa zaidi, ambazo wanaendelea na uzibaji.
“Hakuna daraja lolote lililovunjika wala kumong’onyoka, mawasiliano yapo. Maeneo yaliyoathirika zaidi hasa ni Bonde la Jangwani kutokana na maji kufurika na kupita juu ya daraja kwa muda na Mbezi Kibanda cha Mkaa ambapo barabara ya mchepuko imekuwa na mashimo mengi hivyo kutatiza kasi ya magari na kusababisha foleni na msongamano mkubwa,” alisema.
Hasara
Mhandisi Tenga alisema kwa sasa hawajaweza kufanya tathmini halisi ya hasara iliyotokana na athari hizo, ikiwemo foleni na msongamano wa magari iliyosababishwa na mvua hizi za masika.
Alisema athari zilizotokea sio kubwa kama inavyodhaniwa na wengi na kwamba wanategemea kutumia fedha za bajeti ya kawaida kurekebisha kasoro zilizojitokeza barabarani, isipokuwa tu kwa bonde la Jangwani ambapo athari hii haijaaanza kutokea sasa.
Alisema kwa sasa wanaelekeza juhudi zaidi kwenye suala la kuziba viraka na tayari makandarasi wao wako tayari kwa kazi, ambapo kasi yao itaanza kuonekana dhahiri punde tu mvua zitakapokatika.
Alisema mvua zilizoleta athari kubwa ni za April 2014, Mei 2015 na Oktoba 2017 lakini kwa mwaka huu hakuna uharibifu mkubwa unaofikia wa miaka hiyo.
LUKUVI NA MKAKATI
Aprili 2016, Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema Jiji la Dar es Salaam litafumuliwa na kupangwa upya baada ya Ramani ya Mipango Miji (Master Plan) kukamilika.
Alisema Serikali ipo kwenye mkakati wa kuhakikisha ndani ya miaka 10 ijayo, ardhi yote nchini itakuwa imekamilika kupimwa na kupangwa kwa matumizi mbalimbali.
Kauli hiyo aliitioa wakati akizungumza na wadau wa Sekta ya Uendelezaji Ujenzi Dar es Salaam, ambapo Waziri Lukuvi alisema Jiji la Dar es Salaam linaongoza kwa ubovu wa upangaji miji.
Alisema kwa sababu hiyo, ameagiza kuandaliwa kwa Mpango Mji Mpya ambao utakamilika Julai, baada ya ule wa awali kuoneakana mbovu.
“Mwanzo hatukufanya vizuri. Tuliajiri Consultant (mshauri) wa Master Plan (Mipango Miji) kutoka Italia sitaki kumtaja na yule Mswahili na wengine walioshirikiana nao, lakini kwa ufupi walifanya vibaya. Fedha imekwisha lakini kazi siyo nzuri,” alisema Lukuvi
Mwisho
Dar es salaam kupangwa upya
*Ni baada ya mvua kuharibu miundombinu
Na ANDREW MSECHU
-DAR ES SALAAM