Upendo Mosha, Moshi
Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Marthi Shao,amewataka wanahabari nchini kusimama kikamilifu katika kuandika habari zenye ukweli na uhakika licha ya kukabiliwa na changamoto nyingi.
Dk. Shao ametoa wito huo Leo Mei 25, mjini Moshi, wakati akizungumza katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa mwandishi wa habari na mwakilishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) pamoja na Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW), Nechi Lyimo.
“Wanahabari mnakabiliwa na changamoto nyingi Katika Zama hizi Katika kuandika habari lakini ni lazima mtumie taaluma yenu aliyewapa Mungu na muichochee msiogope changamoto andikeni ya kweli ambayo mnayaamini.
Amesema baadhi ya wanahabari wamekuwa wakipitia changamoto nyingi lakini licha ya changamoto hizo hawapaswi kuacha kuandika Yale Mambo ya kweli yanayotokea Katika jamiii hatua ambayo itaisaida nchi kupiga hatua mbalimbali za Maendeleo