27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ummy Mwalimu awataka wazazi,walezi kusimamia malezi ya watoto

Ramadhan Hassan,Dodoma

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu amewataka wazazi na walezi kusimamia malezi ya watoto wao ikiwemo kuwaogesha ili kuwakagua kama wamelawitiwa ama kuingiliwa.

Kauli hiyo ameitoa Leo Mei 24 bungeni wakati akijibu,swali la Mbunge wa Rombo,Joseph Selasini (Chadema).

Katika swali lake,Selasini amedai kwamba watoto wananyanyasika huku wanaohusika wakiwa kimya, hivyo ni lini Serikali itatembelea mashuleni na kutoa elimu.

Akijibu,Waziri Ummy alisema June 16 mwaka huu ni maadhimisho ya mtoto wa Afrika ambapo agenda itakuwa malezi ya mtoto.

Waziri Ummy ametoa rai kwa wazazi na walezi kutimiza wajibu wao ikiwemo kuwakagua watoto pamoja na kuwaogesha.

“Mimi namkagua binti yangu,waogesheni watoto wenu pale mtajua,lakini mpo bize kutafuta hela mtoto analawitiwa hujui,” amesema.

Katika hatua Nyingine,Waziri Ummy amesema Serikali inampango wa kuanzisha dawati la ulinzi na usalama katika mashule ili wanafunzi wawe na sehemu na kwenda kutoa taarifa wqnapofanyiwa vitendo vya unyanyasaji.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini,Emanuel Mwakasaka(CCM)

Katika swali lake,Mwakasaka alitaka kujua Serikali ina mkakati gani wa kutoa elimu ili watoto wanapodhalilishwa wawe na ujasiri wa kusema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles